Najua chaguao lako ilikuwa Membe, lakini ulipomwaga ugali kwa kumtosa EL, EL friends wakamwaga mboga kwa kumtosa Membe. Bahati nzuri msuguano huu umezaa tunda lenye matumaini walau kwa watanzania wengi. Lakini hata hivyo ilikuwa ujasiri mkubwa saana kumtosa EL. Nakuhakikishia Rais Kikwete kama ungefanya ujasiri kama huu kusimamia rasimu ya Jaji Warioba ikapita kama ilivyoandaliwa kwa kufanyiwa editing kidogo, hakika usingesahaulika milele. Sasa wewe ulidanganywa nawe ukadanganyika ukayasikiliza ya akina kingunge hilo likakuponyoka.
Nakushauri utumia muda uliobaki kuwashawishi wenzako wakubali kurejea mjadala wa katiba mpya, ili tupate katiba inayokubalika na wengi kama ulivyofanikiwa kuvunja makundi ya CCM, sasa uvunje makundi ya wananchi kuhusu katiba mpya, itakuweka pazuri zaidi!