Kikwete Umetumia mimbari kisiasa Rorya!

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Mheshimiwa Rais mstaafu,

Tulidhani ukiishastaafu unatoka kwenye siasa Rasmi, laakini umetumia haki yako ya kikatiba kutoa maoni yako.

Ingawa wengine wanazuiwa kutoa maoni yao ila wewe umetumia mimbari hiyohiyo kufanya kile ulichokipinga.
Ulipaswa kutoa hilo tamko nje ya mimbari hiyo maana hilo sio jambo walilokuwa wamekualika kwenda pale kulisema,ukweli ni kwamba waraka ule umegusa maslahi yako!

Wewe ni mwanasiasa na pale ulikuwa kwenye platform ya kidini, kwa maana kanisa la wasabato.

Kwamba tusichanganye dini na siasa.

Je, Wakati ule ukiusaka u-rais nakumbuka mhashamu kardinali Pengo aliwahi kutamka kwamba wewe ni
"Chaguo la Mungu"

Sikusikia mahali kwenye kampeni zako ukilikemea hilo? Pia huko bungeni wako maaskofu na wachungaji kibao wakifanya siasa,na mfano halisi ni Askofu Gwajima-mbunge wa Kawe.

Je, Mbona wako makanisani wanahubiri na kisha jumatatu wanaenda bungeni pia wanahutubia?

Je! hao mbona CCM iliwapokea na kuwatumia kisiasa mpaka sasa?

Na tena wewe mheshimiwa umenufaika sana kupitia hilo kanisa hadi kukwea na kufikia hapo ulipofika leo.

Bandari isitufanye tukaondoa utu wetu hapa Duniani.



Sauti ya Watu ni sauti ya MUNGU!

Pia, soma
 
Jk amefiliska kihoja
 
Halafu anajifanya yeye ni rais wa nchi huku akimwaga upupu wa kisiasa kwenye mimbari ya dini wakati huo huo anakemea wengine wasitumie!!! Is he serious, he has underrated himself to reclaim the status it may take two centuries.
 
Watanzania hawajaridhika na mkataba wa Bandari yake Salama. Serikali isione aibu kuachana na Waarabu.

Tunaposema Bandari Imegawiwa, maana yake Imegawiwa, tena bure. Wadau wanaodai kuwa kuna rushwa zinanuka kwa kugawiwa Bandari zetu kwa wajomba, maana yake Rushwa inanuka.

Hivi vijisababu na hoja mbovu mbovu walizozitoa na wanazoendelea kuzitoa baada ya kushurutishwa kuhusu mkataba huu, havina maana yeyote ile. Ni uwongo kutaka kuhalilisha Udhalimu na Ufisadi unaotumika kumleta Mwarabu kuja kututawala.

Pinga udhalimu, maangamizo, Ukoloni mamboleo na ufisadi unaofanywa dhidi ya Watanzania,Watanganyika na Wamasai wa Taifa hili kwa nguvu zako zote. Wakemee Vibaraka wote wa Waarabu.
 
Viongoz wa Tz wengi hawajui wanachoongea,wanachotetea etc..
Wengi ni bendera fwata upepo!! Huyu alikuwepo kwenye mambo ya kidini halafu hapo hapo anazungumzia siasa.
Halafu mwisho anasema tusichanganye siasa na dini???

Funny enough:Watu wanapiga makofi eti mstaafu ameonyesha njia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…