Bwana Kikwete ameongea.Kwakweli kila siku anaongea,lakini leo kaongea zaidi maana sikumuelewa.Eti anaita wanasiasa wake 'utitiri'.Kaa!.Kuwaita utitiri maana yake nini,kama si kwamba,kawaona hawana tija.Lakini sasa mbona umechelewa sana?Kwakuwa mambo yameshaharibika!Nathubutu kusema,umekumbuka shuka wakati kumekucha!Lakini angalau hongera ndugu yangu Kikwete kwa kuliona hilo,kwamba jamaa hawa hawana lolote, ingawa kwa kuchelewa sana.Kujua chanzo cha tatizo ni mwanzo wa kulitatua.