Kila aliyefanikiwa na kutajirika anasema alianza kuuza bagia za mia mbili

Kila aliyefanikiwa na kutajirika anasema alianza kuuza bagia za mia mbili

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara (54)✍️
Bila shaka ni kweli, kwasababu sina hakika kama kuna tajiri aliyetamka kuwa utajiri wake umetokana na kurithi/biashara ya magendo/ufisadi/madawa ya kulevya/ujangili/dhuruma/ au kafara.

Licha ya kwamba utandawazi (teknolojia) imetusaidia na inaendelea kutusaidia kushuhudia matukio mabaya (maovu) yanayokamatwa au kuvumbuliwa kwenye jamii, matukio ambayo yanafikirisha sana akili za watu.

Kwa mfano matukio ya watu kuiba kisha kusafirisha meno ya tembo, madini, madawa ya kulevya, ufisadi wa mabilioni ya pesa, dhuruma, n.k.

Lakini kila tajiri anasema alianza kuuza bagia za Tshs 200 akiwa na mtaji wa Tshs elfu moja. Ataendelea kunogesha simulizi yake kuwa alitembeza bagia kwenye sahani kwa miaka kadhaa ndipo alinunua HOTELI, au HEKALI 1000 ZA MASHAMBA, au BUS, au SEMI-TRAILER. Mwisho kabisa anamaliza simulizi yake kwa kusema; "Tunapaswa kuwa na nidhamu ya pesa".

Sina maana ya kwamba matajiri ndio wanafanya biashara haramu. Lakini pia siwezi kusema na sina hakika kuwa biashara kubwa za haramu (Kama usafirishaji wa madawa ya kulevya) zinaweza kufanywa na watu wenye mtaji wa shilingi Laki moja.

Right Marker
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom