Kila aongezewapo Damu huisha, msaada tafadhari

gashambala uwezo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
485
Reaction score
67
Wana jamiiforums naomba msaada wenu;

Shemeji yangu sasa ana kama wiki tatu ni mgojwa sana anasumbuliwa na maumivu makali sana ya kichwa na pili hana nguvu kabisa, tulimpeleka hospitali madakitari walimchukua vipimo, tukaelezwa ana upungufu wa damu, na aliwekewa damu kinachotushangaza sisi akiwekewa damu tu ' kesho yake inakuwa imeisha kabisa na aliweza kuwekewa mara nne yaani chupa 4, na yote inaisha.

Aidha mgojwa amebadilika na amekuwa wa njano, wapo waliotwambia yamukini anaweza kuwa na njano tuliekezwa dawa mbalimbali za kienyeji ametumia lakini ndugu zangu khali haibadiliki, ukimwangalia mgojwa bado ana afya yake kama kawaida, yaani hajapungua.

Mgonjwa hawezi kwenda msalani mpaka awe na mkogojo au mtu wakumushikilia, ana kiu isiyoisha anaku unywa maji mengi sana.

kwa sasa yuko nyumbani, wiki iliyopita alipata kanafuu akaruhusiwa


Jamani hii nini?
 
dalili za 'zombiosis vampirenology' ambapo the victim anakuwa 'zombie'
 
Mkuu umenikumbusha kaka yetu tuliompoteza kwa staili km hii nahic itakuwa saratan ya damu
 
Mkuu kwenye familia yetu yalitukuta kama hayo ni kansa ya damu kaka
Mpelekeni akapme kansa ya damu
 
ndugu hii ni serious insu ,tafuta mtumishi wa Mungu aombewe .rafiki yangu mpendwa alifariki hospitali for the same problem huku munaendelea kumuongezea damu ,tafuta Mtumishi waM Mu au mlete emaus center aombewe.au piga simu namba hii watumishi wa Mungu watakuja kumuombea hapo hospitali0655228899 huo siyo ugonjwa bali nguvu za giza .na hakuna solution hapo waiten watumishi waje kutoa maombi hapo. Ukichelewa mwisho wa siku mutaambiwa ndugu yenu INNI au figo Zimeharharibika, piga hiyo namba haraka mumuookoe ndugu yenu. Pia naomba unipe jina la huyo ndigu ye na mahali alipolazwa ili nimkumbuke kwenye maombi yangu ya usiku wa leo Nipm . Hiyo nmba ni ya mtumishi wa Emaaus Charistmatic prayer Center
 
Wakubwa msi-conclude moja kwa moja kwamba ni kansa ya damu,mgonjwa hajapungua mwili so inaweza kuwa kitu kingine.
 
dooh, umenikumbusha marehemu kaka yetu naye alianza hivyo hivyo baadae akagundulika na kansa ya damu. tena mumuwahishe hospitali mapema. kila la heri.
 
Wahini hospital nyingine kwa wataalam. Endeleeni kumpa mboga za majani hasa tembele, ribena au juice ya rozela kwa wingi. Mpeni pia miwa au juice ya miwa kwa ajili ya njano ila nahisi inatokana.na huo upungufu wa damu. Watumishi wa Mungu msisahau na kama mtafanikiwa na imani nunueni annointing water ya T. B Joshua mumpulizie matone mdomoni ameze huku mkiomba Mungu kulingana kuomba kwenu kwa kinywa chenu na yeye aamini na kukiri uponyaji. Poleni sana.
 
dahaaaaaaaaaaaaaa! Jina lake anaitwa Jonas ombeni Joas, kaka hicho kitu kipo wapi?, aidha mgojwa yuko
Ngara Mkoa wa Kagera.........................Nawashuruni wote kwa ushauri wenu , mwenye mawazo zaidi tafadhali karibu.
 
dooh, umenikumbusha marehemu kaka yetu naye alianza hivyo hivyo baadae akagundulika na kansa ya damu. tena mumuwahishe hospitali mapema. kila la heri.

yaani hospital ni kama vile wameshidwa walitushauri tujaribu mbinu nyingine,
jamaani kansa ngani hii inayotafuna chupa ya damu kwa siku?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…