Wasalaam jamii,
Binafsi nishafanya biashara kadhaa tofauti,
Kuna hii biashara ya kukopesha nguo,viatu nk, ni biashara yenye faida nzuri lakini inachangamoto sana,
Na inahitaji uwe kauzu haswa, pale wateja wakisha kuzoea kukulipa wanakulipa kwa mazoea,
Unakuta mwingine muda umefika wa kulipa deni,atakuambia nikipata nitakulipa,hiyo usihesabie kabisa,
Inafika kipindi bidhaa zimeisha na watu wanahitaji bidhaa na pesa zipo mikononi kwa watu,
Hivyo unaweza ukadai pesa yako na ukajiona msumbufu,
Kama hauwezi kudai hii kitu usifanye,bora uuze ata chakula kikibaki utakula mwenyewe.