Kila biashara ina ugumu wake jamani

Kila biashara ina ugumu wake jamani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Hawa nimiongoni mwa wafanyabiashara wanaokutana na mazingira magumu sana pindi wakiwa kwenye ofisi zao.

Natumaini wengi wetu tumeshakutana au kuona jinsi gani hawa jamaa wanavyofanya hizo biashara zao wakiwa kwenye mishe mishe za kukimbizana na mabasi hususani yale yaendao kwa mikoani.

Ajabu ni pale abiria wanapofanya jambo ambalo linawapa wafanyabiashara hao wakati mgumu pale wanapotaka kununua bidhaa zao, wanachukua bila kutanguliza pesa na kisha wanavizia basi liondoke kisha wanaondoka na pesa ya mfanyabiashara huyo.

Kiubinadamu si jambo jema maana unamrudisha nyuma mfanyabiashara huyo na si kwamba wamkomoa.

Unachoongea ni kweli kabisa mkuu. Ila hata umesahau pia hata abiria huwa wanadhulumiwa chenji zao na wakati mwingine wanapewa bidhaa zilizoharibika. Cha msingi gari kabla halijaondoka liwe linapiga honi ili abiria na wachuuzi wasitishe biashara kuliko kuondoka kwa ghafla.
 
Hawa nimiongoni mwa wafanyabiashara wanaokutana na mazingira magumu sana pindi wakiwa kwenye ofisi zao.

Natumaini wengi wetu tumeshakutana au kuona jinsi gani hawa jamaa wanavyofanya hizo biashara zao wakiwa kwenye mishe mishe za kukimbizana na mabasi hususani yale yaendao kwa mikoani.

Ajabu ni pale abiria wanapofanya jambo ambalo linawapa wafanyabiashara hao wakati mgumu pale wanapotaka kununua bidhaa zao, wanachukua bila kutanguliza pesa na kisha wanavizia basi liondoke kisha wanaondoka na pesa ya mfanyabiashara huyo.

Kiubinadamu si jambo jema maana unamrudisha nyuma mfanyabiashara huyo na si kwamba wamkomoa.

Tofautisha mfanya biashara na mchuuzi. Umeongelea wachuuzi na si wafanya biashara. Title imenivuta kusoma mada yako lakini nilichokikuta ... duh!
Haya ndo matokeo ya '0' za form four katika jamii.
 
muhimu ni wote kuwa waaminifu, hawa wachuuzi nao si wema kivile, kama hayajakukuta unaweza kuwaonea sana huruma, lakini loh! - baadhi wanakimbia na chenji za abiria au kuuza bidhaa zilizooza kama alivyosema mdau hapo juu. Kwa hiyo wakati mwingine abiria anapoondoka na bidhaa bila kulipa ni kama ku-balance vile.
 
Back
Top Bottom