Kila CEO anatamani kampuni yake iwe kama Singapore airlines

Kila CEO anatamani kampuni yake iwe kama Singapore airlines

lanez

Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
78
Reaction score
163
SINGAPORE AIRLINES (SIA), hili ndilo shirika la ndege bora zaidi kwa kutoa huduma kwa wateja, yani ukichukua mashirika yote ya ndege kama British airways, Emirates, air TANZANIA nk, Singapore airline ndio alfa na omega wao kwenye huduma kwa wateja.

Wamefanikiwa kuchukua tuzo nyingi zaidi duniani, kati ya mashirika bora ya ndege, kiasi kwamba kila CEO amekuwa akitamani, angalau nae kampuni yake iweze kufanya kama SIA.

Lakini tukumbuke kwamba hakuna matunda bila uwekezaji wa mzuri, SINGAPORE wanajua kwamba COMPANY PROFITABILITY yani faida ya kampuni lazima itokane na wateja ndio maana wamewekeza sana kwenye huduma kwa wateja.

Sasa angalia uwekezaji wao ulivyo, kwanza moja ya malengo (objective) ilikuwa kuhakikisha kila mteja anayesafiri nao basi hatokaa asahau (wow effects and surpass customer expectations). Wakaja na program ya mafunzo kwa wafanyakazi wao wote (TRAINING), program hii imepewa Jina la TRANSFORMING CUSTOMER SERVICE (TCS)

Kisha wakagawa wafanya kazi wao kwenye makundi 5, la kwanza cabin crew (wahudumu), engineering (mafundi hawa), la tatu ground service (wahudumu wa chini pale), la nne flight operations (wasimamizi wa mambo yote ya usafiri), la tano sales support (watu wa mauzo). Pia wakaja na mfumo wa 40_30_30, hii 40 ya kwa ni watu, 30 ya pili ni uzalishaji na 30 nyingine ni bidhaa.

Sasa ujue kwa nini waliwekeza 40 kwa watu? Kwa sababu uzalishaji na ubora wa huduma unategemea wao ulio nao. Sasa wenyewe wakaamua kuwekeza asilimia 40 ya muda na rasilimali zao kwa watu. Na kilichowekezwa sana ni mafunzo.

Sasa tuangalie mafunzo haya, yalijikita kwenye nini. Ipo hivi, unahitaji vitu vitatu muhimu kwa kila mfanya kazi wako kuwa navyo kama ujuzi (skills). Hata kama huyo mtu kasoma sheria, uhasibu, uwalimu au hajasoma kabisa lakini lazima ajue vitu hivi.

Ajue, huduma kwa wateja (customer service), service management (namna ya kutoa huduma kisasa) na awe na sales skills (ujuzi wa mauzo). Oi hadithi yangu imeishia hapo, utakuza mauzo, biashara yako kwa kuzingatia mafunzo ya vitu nilivyo visema hapa.

Napatikana Instagram @maka__digital, hapo kuna makala nyingi sana, za namna ya kuanza na kufanya biashara


#letstalkbusiness
#letstalkbusiness
#letstalkbusiness
 
Singapore Airlines kwangu naipa no 2 duniani, no 1 naipa Emirates. Naipenda sana sijui kwa sababu inadhamini timu yangu ya Arsenal? Ila thanks mkuu kwa andiko, Singapore Airlines one of the best airlines in the World
 
Hivi unafikir hao CEO wameshindwa kufanya hvyo kama wenzao wanavyofanya

Mambo mengine lazima awepo namba moja hadi kumi na ni mambo mengi tu yanachangia.

Si hizi mbinu pekee
 
Back
Top Bottom