Kila chakula ninachopika hakipendezi

Kila chakula ninachopika hakipendezi

Ben-adam

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
1,043
Reaction score
2,309
Humu kuna wanaume mnajipikia msosi??

Katika vitu vitakavyofanya nioe mapema mojawapo ni hili la mapishi!

Mimi kila nikipika wali lazima uwe mbichi aidha uungue[emoji848] yaani nikiweka moto kidogo, hauivi! moto ukiwa neutral kidogo, unakuwa bokoboko! moto ukiwa mkali, unaungua!![emoji848][emoji848]

Siku moja nilipika tambi! aisee!! ile nimefunika ili zipate moto, nakuja kukutana na uji!! Wanaume mnaojipikia nawapeni HONGERA ya dhati! Mwenzenu vyombo nilishaweka kabatini, na nimeshajipatia umaarufu mkubwa migahawani!

Nawaza waza kutafuta house girl niwe nakaa nae maana natumia hela nyingi kulipia hivi vyakula (hata hapa niko mgahawani) [emoji16]
 
Nunua rice cooker haina kupunguza wala kuongeza moto. Ukipata watoto wa kiume mwambie mama yao awafundishe kupika wasijepata tabu ukubwani
Shukrani sana good idea!
 
Aisee! Tafuta wanao jua kupika wakuelekeze, usione aibu kumuomba mmama au mtu akufundishe kupika.
Ila kwanza jiulize "unapenda kupika kweli?" Then fanyiakazi jibu lako
 
Aisee! Tafuta wanao jua kupika wakuelekeze, usione aibu kumuomba mmama au mtu akufundishe kupika.
Ila kwanza jiulize "unapenda kupika kweli?" Then fanyiakazi jibu lako
asante!

Wazo lako linafaa sana, nimelichukua kama lilivyo
 
Kipindi nipo single nimepika vyakula vyote kasoro pilau tu na mboga za majani.
Chakula changu cha kipekee ni wali nyama(ngombe, kuku, samaki au mzee wa meza.)

Chemsha nyama ikifika 90% kuiva natia mchele, chumvi kidogo, baadae naweka nyanya na kitunguu kidogo. Unapokaribia kuiva na kukauka naweka carrot na hoho za kutosha.
Hakuna kuweka mafuta.
 
Back
Top Bottom