Changamoto na mitihani unayopitia ya kimaisha, yote hayo ni katika kukufanya upanue mawazo zaidi na juhudi ili uweze kufanikiwa. Mungu hawezi kukusahau kamwe,,hiyo mitihani na changamoto unazopitia mungu anataka akufundishe mambo mengi Sana kuanzia kwenye jamii inayokuzunguka Kama majirani,marafiki,jamaa zako,mashosti zako,na watu wengine uliokaribu nao na unaofahamiana nao mpaka kwenye familia yako. huwezi kumjua yupi mwema kwako na yupi ni msaada kwako mpaka upitie changamoto fulani. Hao wote niliowataja hapo juu, wanaweza kuwa wema kwako kama ukiwa na mafanikio(pesa). Utaona wakiwa karibu na wewe, wakicheka na wewe,wakijionyesha kukuthamini Sana lakini kumbuka hapo ni kwakua pesa yako imekuziba usiwafahamu kiundani kwenye mioyo yao. ila fumbo kubwa ni pale kwenye matatizo, Hapo utashangaa masimango,dharau,kejeli,matusi,n.k utayapata kwa hao wote niliowataja,isipokuwa sio wote watakao fanya hivyo. Ni vigumu kujua mioyo yao inawaza nini.
Kumbuka mungu anakuacha upitie hayo yote ili akufunze na aipanue akili yako ili baadae akikufungulia milango ya baraka, utakuwa umeshajifunza mambo mengi na kuona mengi kwenye jamii na familia yako kwa ujumla.
Kumbuka:
Kuwa mvumilivu na mwingi wa Kusali.
Mshukuru mungu kwa kila hatua uliyopo,hata kama una shilingi sifuri mfukoni,endelea kumshukuru tu, maana hapo ndo kipimo cha kumjua yupi Real kwako na yupi fake kwako.