Kila jambo ukilichukua kama funzo utaenda mbali zaidi

MwakiIV

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
79
Reaction score
138
LAWAMA HAIJAWAHI KUPONYA MTU.

Mara nyingi tumekuwa tukilalamikia vitu ama watu lakini tumeweza kujiuliza kwa nini vitu au watu hao utokea kwenye maisha yetu?

Mtoto anazaliwa mara ya kwanza hewa ya oksijeni inapopita kwenye mapafu uanza kulia na baadae ataitegemea hiyo kwa maisha yake yote.

Vijana tumekuwa tukiamasishwa kujitolea na kushiriki katika fursa tofauti, ambapo ukitazama juu juu ni kama unapoteza muda lakini ukichukulia kama funzo kipo utakachopata ambacho kitakusaidia mbeleni.

Wakati mwingine hata tukivuta taswira ya namna tulivyolelewa utagundua ukali wa wazee ambapo wengine tulidhani ni maonevu lakini leo tunafurahia matunda yake.

Ugumu wa jambo ni njia rahisi sana ya kujifunza jambo lenyewe lakini kama utalibeba kwa mlango wa chanya.

Hivyo namalizia kwa kusema hakuna sehemu ulipoteza muda, hakuna mtu alikupotezea muda yote hayo ukiyataza kwenye mlengo chanya utakuta kuna funzo bora umepata.
 
Tatizo maisha yetu hayawezi kujibiwa na jibu moja.

We tuache tu mtu naondokewa na wapendwa wangu ati ni funzo?!!?
 
Pole sana na ni kweli hatuwezi kuwa na jibu kwenye changamoto.
Lakini Lawama sio suluhu.
Pia ukosapo wapendwa wako inaweza kuwa chachu ya wewe kwenda mbali zaidi.
 
LAWAMA HAIJAWAHI KUPONYA MTU.

Mara nyingi tumekuwa tukilalamikia vitu ama watu lakini tumeweza kujiuliza kwa nini vitu au watu hao utokea kwenye maisha yetu?

Mtoto anazaliwa mara ya kwanza hewa ya oksijeni inapopita kwenye mapafu uanza kulia na baadae ataitegemea hiyo kwa maisha yake yote.

Vijana tumekuwa tukiamasishwa kujitolea na kushiriki katika fursa tofauti, ambapo ukitazama juu juu ni kama unapoteza muda lakini ukichukulia kama funzo kipo utakachopata ambacho kitakusaidia mbeleni.

Wakati mwingine hata tukivuta taswira ya namna tulivyolelewa utagundua ukali wa wazee ambapo wengine tulidhani ni maonevu lakini leo tunafurahia matunda yake.

Ugumu wa jambo ni njia rahisi sana ya kujifunza jambo lenyewe lakini kama utalibeba kwa mlango wa chanya.

Hivyo namalizia kwa kusema hakuna sehemu ulipoteza muda, hakuna mtu alikupotezea muda yote hayo ukiyataza kwenye mlengo chanya utakuta kuna funzo bora umepata.
_ (3).jpg
 
Back
Top Bottom