Kawavuta wapinzani waliohamia CCM kawapa nafasi za kugombea kwenye majimbo waliyokuwa wanayaongoza wakiwa Upinzani. Wakabweteka na wengi wakahama na kupewa maisha na mkuu.
Mwaka huu akawaahidi bonge la BOKO kwamba waliohamia wapitishwe na wasibughudhiwe na wanaccm.
Akawaonya wateule wake wasigombee ubunge waridhike na nafasi alizowapa.
Wasaliti kama kawaida yao wakashupaza shingo wakaenda woote kugombe wakiwa na fikra kwamba wao ni EXCEPTIONAL yaani wana BOKO lao kibindoni.
Walipojiudhuru nyadhifa zao JPM akaziba mapengo faster.
Huko kwenye vikao vya Chama wajumbe wakawasha moto kwamba hakuna mtu "kubebwa"(BOKO) kila mtu akapambane kivyake. (Kumbuka wameshaachia madaraka?)
Wakazama kwenye majimbo wakaangukia pua wote kasoro wa Sia aliyetofautiana kura moja na A. Mwanri (huyu ataangukia pua huko aendako)
Yaani JPM ameonesha ushujaa wa hali ya juu kwa hawa walafi wa madaraka sasa wavae tu mashati ya kijani bila senti mfukoni.
mliobakia jifunzeni kwa wenzeni.
NB: Wenye kijani halisi ni waliokulia chamani sio wahamiaji