Kila kitu bongo kipo tofauti

Kila kitu bongo kipo tofauti kwa sababu kuna CCM na serikali yake.
 
Kwa wenzetu mtu mwenye afya ni yule anayekula vizuri na kufanya mazoezi, Bongo mtu mwenye afya ni yule Mnene kuliko wote anayekula vya 'kurosti'
 


HEBU SUBIRI KIDOGO....
Sidhani ni rahisi kama unavyoonyesha kwenye kuandika.
Tueleze ni jinsi gani haya mabadiliko yatafanywa.Yote uliyoyaonyesha yanafahamika - it is the HOW PART ndio bado hatujajua.
tuepuka kutoa majibu mepesi kwa matatizo magumu.
 


Naona hatukuelewana kidogo. Mimi niliandika kuwa kazi za serikali TZ siyo kazi ya wito kama ambavyo ingetakiwa iwe. Lakini wewe umeandika kinyume. Tanzania watu wanataka kazi serikalini ili kusawazisha maisha yao binafsi. Kuna mifano mingi ya watu waliotajirika serikalini bila hata kuwa na kazi katika sekta binafsi maisha yao yote. Mfano mzuri ni Chenge na Lowasa.
Nchi zilizoendelea kazi za serikali ni kazi za wito, Watu wanaenda serikalini to pay back to the society. Mfano mzuri ni gavana wa California ambaye nafikiri mshahara wake ni dola 1 [moja] kwa mwaka. Mayor wa NY naye ni hivyohivyo.
Rais wa USA mshahara wake ni $ 400,000 kwa mwaka.Yeye ana degree ya Law ya Harvard, angeweza kuingiza hela nyingi zaidi ya hapo kama angekuwa kwenye private practise. Hasheem Thabeet kwa mwaka mmoja atakuwa analipwa mara 8 zaidi kuliko US president.
Point ni kwamba serikalini siyo sehemu ya kutajirika ni sehemu ya kuhudumia jamii.Haina maana eti kwa sababu Bloomberg halipwi mshahara basi ni bogus, wananchi wa NY wameridhika naye mpaka wamebadilisha sheria za uchaguzi ili agombee tena.

Huu ni muono wangu.
 

Hapa ndipo nchi yetu inapokwama. Vikao vingi sana, semina nyingi sana, tume nyingi sana. Na tume inaundwa kupitia maazimio ya tume iliyopita !!!Tusifanye vitu kuwa vigumu namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…