Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Kikosi cha Simba kimeondoka jioni ya leo kuelekea nchini Misri kwenye mchezo wa marudiano siku ya jumanne.
Wengi wametoa tathmini zao, wengine wakimshambulia Somba Onana wakisema hana hadhi ya kuchezea Simba, wamesahau kuwa hata Kibu Dennis walimsema hivyo hivyo na Leo anaonekana ndio mfariji mkubwa ndani ya Simba.
Wengine wamemlaani Kocha kwa mabadiliko aliyoyafanya hasa kumuingiza Onana na Bocco lakini wamesahau kuwa Bocco ndio huyo huyo alimlazimisha beki wa Power Dynamo kujifunga pale chamazi na kutupa tiketi ya kucheza makundi.
Wengine wamedai Fabrice Ngoma kuwa ndie nyota wa mchezo lakini hv majuzi tu kule Singida walisema Fabrice ni slow sana, haendani na kasi ya Simba.
Wengine walikuwa wanaombea mungu Inonga apone mapema ili akiwashe na Al Ahly lakini jana wamedai kumkumbuka Kennedy Juma.
Wengine walikuwa waiimchukia Kanoute wakisema amechoka na hana uwezo lakini jana wamebadilika wakisema alipoingia mchezo ulibadilika.
Basi ali mradi kila mtu ana haki ya kutoa maoni wametoa.
Wengine wamesema jana pale uwanjani kuwa Al Ahly ni maji ya shingo, wako level ya juu sana ila wamesahau kuwa Al Ahly na Wydad wako level moja na Simba ilimkazia Wydad huko huko kwao.
Wamesahau kuwa Leo Al Ahly wameiomba mamlaka iruhusu mashabiki kuujaza uwanja na hawataki tena ile idadi ya mashabiki 30,000 waliopangiwa, wameona sio jambo la kawaida kwao hasa kuruhusu mabao 2.
Al Ahly wametafakari sana kwann Simba wamepata mabao 2, kama walipata mabao kwal hawawezi kukosa mabao huko huko kwao pia, wanaiona Simba ni tishio kuliko dharau zinazofanywa na baadhi ya watu kwa timu hiyo ambayo imemfanya Injinia Hersi adandie treni kwa kuonekana huko kigamboni akiwa na Rais wa FIFA.
Kila la heri mnyama, msisikilize makelele ya watu, mpira umeshavamiwa huku bongo, mimi ni mmoja wa wanaoamini kuwa jumanne dunia itasimama huko nyumbani kwa mafarao.
Safari njema na mungu awabariki sana.