FBY 2013
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 401
- 90
Ikiwa imebaki takribani siku Moja ili Bunge Maalumu la Katiba lianze vikao vyake Huko Dodoma,Wananchi wamekua na Mitazamo tofauti tofati kuhusu Bunge hilo.
Wapo waliosema kua Chama tawala kina Wajumbe wengi zaidi hivyo kwa asilimia kubwa Mambo yote yanayoungwa Mkono na Chama hicho yatapitishwa huku Masuala Mengine ya Msingi ambayo chama hicho hakiyakubali yakipindishwa.
Wapo pia waliosema kua Karibu asilimia 80 ya Wajumbe wa Bunge hilo ni wanasiasa hivyo kuna uwezekanao Mkubwa wa Mijadala Kutawaliwa na Hoja za kisiasa huku wakiacha Masuala mengine muhimu yenye Maslahi Mapana kwa Ustawi wa Nchi yetu.
Wapo waliosema kuna Baadhi ya Wajumbe Hasa Wabunge wa JMT Watakua wasinziaji huku wakishtuka na Kupiga Makofi makubwa ilihali hawajui wala hawafatilii kinachojadiliwa wakati huo ilimradi na Wao wamo Kisha wajipatie posho zao Nono zilizotengwa kwa ajili yao.
Pamoja na Mitazamo hiyo na Mambo Mengine Mengi bado hatukomi kuwalilia Wajumbe waliopata Nafasi hiyo nyeti inayopelekea kuweka Historia Kubwa katika Nchi yetu.
Tunatambua kua Mchakato huo umeligharimu Taifa kiasi kikubwa sana Cha Pesa mpaka kukamilika,Pesa ambayo ingetumika kujenga Hospitali nyingi na Kununua vifaa vya Tiba hali ambayo ingepelekea Kuokoa Maisha ya Watu wengi.
Pesa amabyo ingenunua Vitabu vingi,Madawati ya Kutosha,Vifaa vya Maabara na Kuwalipa Walimu Madeni yao hivyo kuinua Kiwango cha Elimu katika Nchi yetu.
Pesa ambayo ingeweza Kufanya Mambo Mengine Mengi ya Maendeleo katika Nchi yetu hii inayolalamika kila siku Kua ni nchi Maskini kumbe ni Umsikini wa Kujitakia wenyewe!
Kwa Mantiki hiyo basi.
Tunatoa Wito kwa Wajumbe wote wa Bunge la katiba kutambua ya Kua:
Wamepewa Dhamana kubwa ya Kufanikisha au kutofanikisha adhima ya Upatikanjai wa katiba Yenye Maslahi kwa Wananchi na Hivyo waijadili Rasimu hiyo kwa Busara,Weledi bila kuweka Maslahi ya Vyama wanavyotoka bali waiangalie Tanzania Baada ya Miaka 100 ijayo.
Watambue Watu wengi Makanisani Na Misikitini wanaombea Mchakato huo ukamilike na kuleta Katiba yenye Maslahi ya wananchi,Kilio cha Wengi ni kilio cha Mungu hivyo wawe Makini endapo wataweka Maslahi yao na Kusahau mambo Muhimu,HAKIKA ADHABU YA MUNGU HAWATAIEPUKA.
Watambue kua wanaenda Kuboresha Rasimu ambayo kwa Kiasi kikubwa yaliyomo ni Maoni ya Wananchi Wengi hivyo hatutarajii kuona Mabadiriko makubwa sana.
Mwisho kabisa Tunawatakia kila la Heri,Mungu awaongoze kwa Hekima na Busara zote,Mungu awajalie Afya njema wakati wote.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu Bariki Mchakato wa Katiba Mpya.