Kila la kheri Mwaka wa Kwanza!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Pazia la mwaka wa masomo wa 2012/2013 vyuoni linafunguliwa kesho ambapo UDSM inapokea wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Kesho na muhula mzima wa kwanza patajaa vituko na ushamba wa kila aina. Ni mambo ya kawaida lakini. Cha muhimu ni kuwa vyuo vinafunguliwa na masomo kuanza. Maisha yanaendelea. Kila la kheri M4C wote!
 
Nimekutana ubungo na mwanafunzi wa mwaka kwa kwanza udsm katoka kigoma asubuhi hii eti ananiambia nimuonyeshe sehemu ambayo ataweza kuoga na kubadili nguo eti amechafuka na vumbi la safari mimi nikamuelekeza mahali ambapo kuna mabafu ya kulipia ndio aende huko
 
shukran mkuu japo inawahusu watu wa udsm.....
 
ngoja niendelee kukaa hapa hapa ubungo ikiwezekana hata niwapige picha hawa wanafunzi wa mwaka wa kwanza udsm wamikoani jinsi walivyo chafuka na vumbi la safari
 
Nimemkamata mwingine kashuka kwenye sumry ya bukoba eti ananiomba msaada nimwelekeze sehemu kunakouzwa nguo eti hawezi kwenda udsm na nguo zake za zamani eti anadai zimechakaa atachekwa na wasichana wa udsm
 
Hii kali sasa
 
teh. . .!
 
Mpiga msuli yupo kazini,, acha majungu kijana kafanye kazi tujemge nchii hii, huo ushamba wa muda tu wape semister moja tu watakuwa wajanja na swaga zaidi yako
 
Nipo hapa dukani kwangu mara kaja jamaaa anatokea kibondo kata ya nyaronga kigoma anakwenda udsm akataka kununua maji ya kunywa ya litamoja nikamwambia litamoja 2500, akatoa dah nikasema leo na wiki hii nitatengeneza faida kubwa hapa dukani kutokana na wanafunzi wa mwaka wa kwanza udsm
 
Utaua Mkuu
 
mweeeeeeeeeeeeeeeeee. kila la kheri vijana.... najua vijana watakuwa wanatembea mwendo mdundo, si unajua karibu mjini
 
ngoja niendelee kukaa hapa hapa ubungo ikiwezekana hata niwapige picha hawa wanafunzi wa mwaka wa kwanza udsm wamikoani jinsi walivyo chafuka na vumbi la safari
lakin mkubwa badala ya kujiandaa kwenda MUCCOBS unakaa unashangaa watu wa udsm...duh mkubwa acha na mimi nikae hapa moshi stand nikucheki utavyong'aa mimacho...na ukizubaa tunakuvua mpaka viatu!!!!!
 
unajiona mjanja,ngoja uende huko Moshi ukakutane na WAMENYA wakuaibishe,chezea Moshi
 
Ahsante mkuu ila nina mzuka na kushika peni si mnajua sijapiga nyanga kitambo. . .
 
Ahsante mkuu ila nina mzuka na kushika peni si mnajua sijapiga nyanga kitambo. . .

Utakul extreme 2 weeks hadi utachoka mwenyewe, labda uwe mzoefu ka mimi extreme kwangu kitu ndogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…