Kila la kheri Yanga Jumamosi

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika mchezo wake wa jumamosi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) dhidi ya timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika salamu zake kwa klabu ya Young Africans, Rais Malinzi amewaambia wanapaswa kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa jumamosi, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano kwani ndio pekee kwa sasa wanaoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa.

Young Africans imeingia katika hatua ya 16 bora Kombe l Shirikisho barani Afrika,baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao (3-2), kisha kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao (5-2).

Endapo timu ya Young Africans itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia kucheza mechi ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo zitakaotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).

Wakati huo huo wapinzani wa Young Africans timu ya Etoile du Sahel wanatarajiwa kuwasili saa 9 usiku kuamkia ijumaa kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia (FTF), Bw. Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Bw.Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10.

Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na kesho jioni ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na wanatarajiwa kuwasili leo mchana, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA KHAMIS MCHA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetuma salamu za rambirambi kwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Khamis Mcha kwa kufiwa na baba yake mzazi Mcha Khamis.

TFF inampa pole Khamis pamoja na familia yake, ndugu,jamaa, marafiki na klabu ya Azam FC na kusema iko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, marehem Mcha alifariki dunia juzi kisiwani Zanzibar.

VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho siku ya ijumaa kwa mchezo mmoja, wenyeji timu ya Stand United watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, mjini Morogoro wenyeji Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Jijini Mbeya wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamanzi Complex.

Jumapili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea kwa maafande wa timu ya Ruvu Shooting kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mabatini - Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar.

NB: Kesho siku ya ijumaa saa 5 kamili asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa mikutano wa TFF - Karume

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Baraka Kizuguto,

MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
 
Naamini kocha wa Yanga amewaweka vizuri kisaikologia wachezaji. Sioni tatizo lingine ili kuweza kuwafunga hao waarabu.
 
Yanga piga hao Waarabu. Hata ukuta wa Yeriko ulidondoka.
 
Naomba Yanga wafungwe na Etoile Du Saleh

Na ni lazima wapigwe tu
 
Bwana yupi? kanjibhai manji au?

bwana mungu muumba wa mbingu na dunia, na vitu vyote .... ambaye kwa yeye tunafanikiwa maombi yetu na kwa maombi yetu wana yanga, mungu ametusikia akatufikisha hapa tulipo na tunaendelea kumuomba ili tushinde......kwa uweza wake tutashinda...EE MUNGU TUSAIDIE.
 

Hakuna kitu mkuu....huyo bwana unayemtaja hahusiki na Yanga
 
Mechi ngumu sana hiyo jumamosi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…