Kila mkoa kuwe na eneo maalum la walemavu

Kila mkoa kuwe na eneo maalum la walemavu

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Huwa napata uchungu sana pale nikiwa natembea bara barani halafu nakutana na mtu mwenye ulemavu akiwa na bakuli anaomba omba,

Wazo langu kwakuwa sisi watanzania hatunaga baya pale tunapoona serikali inatoa msaada basi serikali itenge maeneo maalumu ya watu hawa na iwatengenezee miundombinu ya kilimo ufugaji na nk.

Sababu vilema wapo wa aina tofauti mfano asiye na miguu anayo mikono asiye na macho anayomasikio, na hii itakuwa ni kwa wale tu wasiojiweza ila nguvu na akili wanazo,

Pia kutakuwa na vigezo vya mtu kuingia kule

Japo najua changamoto hazkkosekani hasa pale watakapokuwa wamepata watoto na watoto watakapokuwa wakubwa itakuwaje?

Najua serikali ina wasomi wengi hawatakosa namna ya kufanya,

Nawasilisha hayo ni maoni yangu tu

Wanateseka sana wanahitaji huruma ya serikali.
 
Back
Top Bottom