Mamshungulii
Senior Member
- May 3, 2023
- 175
- 88
RISASI MBILI
Kuna kisa kimoja kuhusu “risasi mbili” CHEUSI, muuaji, mpiga risasi ambaye havuti wala halewi, alikuwa ameenda Masaki kutembelea nyumba ya mpenzi wake karibu na barabara ya Chole. Zaidi ya maaskari 100 wakiwa chini wamelenga ghorofa ya juu, walipiga risasi kwenye ukuta, wakijaribu kutaka kumpiga risasi CHEUSI, ”muuaji wa polisi” walizingira na kufyatua risasi eneo lote ni vipande vya risasi nakelele zake zilizokuwa mtaa mzima na mahsusi kwenye jengo aliloko Cheusi kwa takribani saa nzima. Cheusi akiwa amekaa kwenye kiti juu akipiga risasi watu wengine wajasiri wakiwa wanashangaa kinachoendelea hapo mtaani.
Kamanda wa polisi eneo hilo alisema CHEUSI ni moja kati wa jambazi na gaidi hatari kutokea katika himaya hiyo” Ataua na ana malengo ya kuua”, alisema kamanda akiwa anahabarisha wanahabari.
Lakini Cheusi yeye anajionaje, tunatambua maana wakati mapolisi wanafyatua risasi kwenye jengo alipokuwa yeye, aliandika barua iliyosema “KWA YEYOTE ATAKAYEHUSIKA” aliiandika kwa kutumia damu kutoka kwenye jeraha la risasi. Katika hii barua Cheusi alijisemea,” ndani ya koti langu kuna moyo uliochoka, lakini mpole, ambao hautamdhuru mtu yeyote.”
Cheusi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, alivyofika wakati wa kunyongwa alisema hivi ”Hii ndio zawadi yangu kwa kuua watu?" Hapana: akasema hiki ndicho nakipata kwa kujitetea dhidi ya kifo.” Hapa Cheusi hakujilaumu kwa lolote, akaendelea kusema nimetumia miaka bora ya maisha yangu kuwapa watu starehe, kuwasaidia kuwa na wakati mzuri na nilichopata ni unyanyasaji, na kuwindwa kama mnyama.
Nilikuwa na maongezi mazuri na wafungwa wa gereza la Butimba baada ya kuwekwa ndani kwa makosa ya mauaji, mahabusu na wafungwa hapa Tanzania wengi wao wanajiona kama watu waso haki, ni binadamu kama wewe na mimi Wanafikiri, wanajielezea, wanaweza kukuambia kwa nini walilazimika kuvunja salama au kuwa wepesi kwenye kidole cha kufyatua risasi. Wengi wao hujaribu kwa njia ya kufikiri uwongo au kimantiki, ili kuhalalisha matendo yao yasiyo ya kijamii hata kwao wenyewe, kwa hivyo wakisisitiza kwamba hawapaswi kamwe kufungwa kabisa.
Kama Cheusi na baadhi ya wafungwa wanawake na wanaume waliopo gerezani hawajilaumu chochote kwa lolote, vipi kuhusu watu ambao mimi na wewe tunakutana nao kila siku?
Zaidi ya miaka 30 kwenda nimejifunza kuwa ni upumbavu kuadhibu. Inaniwia vigumu kuyashinda mapungufu yangu bila kuhangaika juu ya ukweli kwamba Mungu hajaona inafaa kugawa sawasawa zawadi ya akili. 99% ya watu hawajiadhibu kwa lolote, haijalishi kosa liko kwa namna gani. kuadhibiwa kunamweka mtu katika kujilinda na kwa kawaida huwafanya kujitahidi kujitetea. Kuadhibiwa ni hatari, kwa sababu kunaumiza nguvu ya thamani ya mtu, huumiza hisia zao za kujiona wana umuhimu, na kuamsha chuki.
Wanazuoni wanasema Mnyama ambaye anazawadiwa kwa mazuri atakuwa mbora zaidi kulikoni mnyama ambaye atahukumiwa kwa mabaya na hii ni sawa kwa wanadamu wote. kwa kuadhibu hatufanyi mabadiliko ya kudumu na mara nyingi huleta chuki. kadiri ilivyo kiu ya kupata kibali, kuogopa kulaaniwa
chuki ambayo hutokana na kukosolewa au kuadhibiwa inaweza kuwavunja moyo wafanyakazi, wanafamilia na marafiki, na bado isirekebishe hali hiyo.
Chapakazi ni afisa usalama katika kampuni ya uhandisi, moja kati ya wajibu alionao ni kuhakikisha mafundi wanavaa kofia ngumu mara zote wanapokuwa kwenye kazi. Na mara zote akienda kukagua huwaambia kwa maneno ya mamlaka na ukali kwamba ni lazima wavae kofia hizo za ujenzi na kwa uzuri mbele yake wanatii na kuvaa ila punde tu aondokapo wafanyakazi wanarudi kwenye yale yale. Yaani wanavua kofia. Mkama akaamua kubadilisha mbinu tofauti, wakati mwingine anapowaona wafanyakazi hawajavaa kofia ngumu anawaliza kama kofia hizo haziwatoshi au zinawabana halafu kwa upendo anawaambia kofia zimetengenezwa kwa ajili ya kulinda usalama wao ili wasidhurike. Na majibu yaliongezeka na mbadala ufuatiliaji wa sheria ulikuwa mkubwa pasipo ushambuliaji wa hisia za watu.
Mr Cheupe katibu wa kampuni ya mambo ya ndani, alikodisha sehemu ya kuvuna mafuta ambayo yalitakiwa yatumike kwa mustakabali wa taifa wa baadae, lakini secretary hakuruhusu mnada wa wazi? Hapana alimpa rafiki yake huo mradi Mr Chekundu, na Mr Chekundu alipokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa kigezo kwamba wamekopeshana, na wakawaamuru wabia wengine wasiingie kwenye ushindani kwani tayari mr chekundu kashakabidhiwa. Wabia hao baada ya kutokuridhika na hicho kitendo wakaamua kwenda mahakamani na kuiweka habari hadharani. Dili likawekwa wazi, taharuki mitandaoni na mjini, mfumo mzima wa taasisi ya cheupe ukavurugika na kutishia kwenda kukiachia chama alichopo cheupe na kumuweka Mr Cheupe gerezani.
Cheupe akahukumiwa, akadhihakiwa kana kwamba yeye ndio wakwanza kukosea. Je ametubu? Hapana! Baadae viongozi wengine wakasimama na kusema mambo mengi yamedhorota sababu ya matendo ya Mr Cheupe. Hakuwa kiongozi mzuri. Ghafla mtoto wa Mr Cheupe akasimama akawaambia ”Baba yangu hakuwahi kumsaliti yeyote. Hili jumba lililojaa dhahabu lisingeweza kuruhusu baba yangu afanye hivyo. Nyinyi ndio mliomsaliti baba yangu na mkapelekea ajiue. Hapa sasa, asili ya binadamu katika matendo, watenda maovu, hulaumu kila mtu lakini sio wenyewe. Sasa mimi na wewe tupoje? Lini mimi na wewe tukitaka kumlaumu mtu kesho tukumbuke “RISASI MBILI“ cheupe na cheusi.
Kukosolewa ni kama njiwa wa nyumbani, aondokapo hurudi tu, tuseme kwamba mtu tunayemkosoa na kumlaumu, atatafuta namna ya kujitetea na kutukosoa na kutulaumu. Tunapofanya kazi na watu tuelewe ya kwamba malezi yetu ni tofauti, historia zetu ni tofauti, tumeumbwa kwa kutumia hisia na sio fikira pekee.
SIRI KUBWA YA KUFANYA KAZI NA WATU
Kuna njia moja ya kumfanya yeyote afanye chochote, umewahi kufikiri hili? Ndio njia moja na ni kumfanya mtu afanye kile anachokitaka. Na si kingine zaidi ya ‘Hitaji la kuwa wa muhimu’ na baadhi ya vitu ambavyo wengi na kila mwananchi hupenda ni kama ifuatavyo:
1. Afya na ulinzi wa maisha
2. Chakula
3. Usingizi
4. Hela na vitu ambavyo hela imenunua
5. Maisha baada ya dunia
6. Furaha ya kimahusiano
7. Ustawi wa watoto wetu
8. Kutambulika na kuonesha umuhimu wetu
Kila mtu anapenda kushukuriwa, kuonekana ni wa muhimu, anashukuriwa, anasifiwa, anapewa kipaumbele. Ni hitaji hili la kuwa wa muhimu linalofanya watu watake kuvaa nguo zinazoenda na wakati, kuendesha magari mapya, na kuongelea kuhusu yule binti au kijana mtanashati.
KUWA KIONGOZI WA KUBADILI TABIA NA MITAZAMO KWA:
1. KUPONGEZA NA KUSHUKURU
2. KUKOSOA WATU WAZIMA KWA TAFSIDA
3. KUJIKOSOA KABLA YA KUKOSOLEWA
4. ULIZA MASWALI KWANZA KABLA HUJAANZA KUAMURU
5. TUNZA SONI ZA UNAOFANYA NAO KAZI NA UNAOWAONGOZA
6. MPE MTU SIFA NJEMA YA KUISHI NAYO
7. PONGEZA VIDOGO HATA VIKUBWA
8. HAMASISHA, MFANYE MTU AFURAHIE KUFANYA ULIVYOPENDEKEZA

Upvote
1