Kila mtu ashinde mechi zake: Mr Blue ni king of stage(mfalme wa jukwaa)wasanii wana la kujifunza

Kila mtu ashinde mechi zake: Mr Blue ni king of stage(mfalme wa jukwaa)wasanii wana la kujifunza

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi
Katika moja ya changamoto kubwa kwenye biashara ya muziki na burudani kwa sasa ni wasanii kuweza kuwafurahisha mashabiki mwanzo wa show hadi mwisho hata kama msanii hana wimbo mpya.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wasanii wetu wa bongo fleva ni wachovu kabisa jukwaani tena ni watu wanao boa kabisa wakipanda jukwaani na ni bora ukasikiliza radio kuliko kuwasikiliza wakiwa jukwaani.

Wasanii wetu wamezoea kuimba juu ya wimbo na hawana pumzi kabisa hata za kuimba dakika 20 badala yake ni kupiga kelele na mashabiki wanabaki wana waangalia tuu.

Kuna muda mwingine msanii anapanda jukwaani anaimba wimbo ambao ni maarufu hadi watu wanaanza kuulizana ni huyu aliyeimba au mwingine?

Hapo zamani kabla ya ujio ya mziki wa singeli kwenye main stream ukweli wanamuziki wa hip hop walikuwa hawana mpinzani kabisa kwenye majukwaa lakini kwa sasa wanapata upinzani mkubwa sana wanapo kutana na wanamuziki wa singeli ni wana hip hop wachache sana kwa sasa wanaweza kubatle kwenye jukwaa moja na wasanii wakubwa wa singeli.

Lakini pamoja na hayo yote Msanii Mr blue ndiye msanii ambaye anao uwezo mkubwa sana stegini na pumzi kubwa stejini na ni ukweli usiopingika ni msanii pekee ambaye aweza kupambana na wasanii wa singeli katika kuwateka mashabiki na kuimba nao

Pengine Mr Blue aongelewi sana kwenye maradio na kwenye mitandao ya kijamii lakini ndiye msanii anayekubaliki sana majukwaani na mashabiki na kama kuna mtu aliwai tazama show yeyote ya Mr Blue au kuhudhuri matamasha atakubaliana nami kuwa Mr Blue ni mfalme wa jukwaa kwa sasa.

Pengine watu wanaweza wasikubaliane nami lakini tunaomba tuulizane kama kuna msanii wa sasa mwenye pumzi stejini kama Mr Blue.

Baada ya kumuangalia jana kwenye mziki mnene ya EFM aliendelea kunithibitishia kuwa yeye ni mfalme kabisa wa stageni na pia pengine Dares-salaam ni base yake kabisa.

Wasalaam
 
Mr Blue Collabo za wenzake anawafunika sana,Shetta ft Blue,Rayvanny,Hatufanani nao,Nyandu ft Blue,Jux zote kafunika.

Sometimes najiulizaga anakoseaga wapi sijui jamaa upande wa kuswitch flows hamna anayemgusa.
 
Mr Blue Collabo za wenzake anawafunika sana,Shetta ft Blue,Rayvanny,Hatufanani nao,Nyandu ft Blue,Jux zote kafunika.

Sometimes najiulizaga anakoseaga wapi sijui jamaa upande wa kuswitch flows hamna anayemgusa.
Hakika
 
Blue ni mzuri na consistency yake kwenye game ni ya hali ya juu.

Overall tusipo categorise aina ya mziki mimi binafsi nawaelewa zaidi TID na Rubi linapokuja suala la stage

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana Harmonizer sijui alikua anaongea vitu gani,anasema masela mtu asie vua shati hapa uwanjani mle denda,mara mtu asiyenyoosha mkono juu mtongoze.

Sent using Jamii Forums mobile app
Harmonize wa sasa hivi ndo ana potray tabia halisi ya wamakonde,hivyo ndivyo tulivyo....tuna ulimbukeni flani.....(refer hela za korosho mbuzi kulishwa chapati kwa soda)😁
 
Huwa ninawapongeza sana watu wanaohudhuria hizo shoo....
 
Back
Top Bottom