Kila mtu hufurahi akiambiwa "Mtoto Huyu Kafanana na Baba Yake"

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Kinababa hufurahi sana wakisikia kuwa wamefanana na baba zao, hali kadhalika nasi kina mama hufurahia kusikia watoto wetu wamefanana na Baba zao.
Hii inatujengea imani kwa wanao tuzunguka kuwa hatujachakachua
 
kinababa wengi huchukia wanapoambiwa mtoto kafanana na mamake!!
 
Mwanangu huyu wa mwisho alipokuwa na umri wa miezi hadi miaka miwili alifanana sana na muuza Genge wa hapa jirani kiasi ilikuwa tabu kubwa kwangu. Ajabu sasa ana miaka minne anafanana nami dhahiri hata mwenyewe nakiri kafanana nami... Ila shaka yangu juu ya muuza genge ingalipo japo namwamini mke wangu.
 
mhhh...sasa kama mtu mwenyewe ni wa kusafiisafiri halaf ukazaa moto akafanana na mtu mwingine unadhani itakuwaje? kila mtu hufurahi akiambiwa anafanana na mwanae
 
mbaya zaidi ukiambiwa mtoto kafanana na bosi wako..
 

hahaha mna kazi kweli.

Mie mwanangu binti nitaomba Mungu asifanane na baba yake! mtoto wa kike sura ya kiume iweje?
 
ina raaaha gani mtoto anaonekana kabisa hafanani na babaye, lakini watu wakakwambia kuwa mtoto huyu kafanana na baba yake?
 
waswahili akikwambia mtoto kafanana na baba yake anamaanisha mwanao ana sura mbaya!
 
Kuna mtoto nilienda kumwangalia wazazi wake wakaniomba opinion yangu kwani walikuwa wanabishana kila mmoja anasema amefanana nae; mimi nikawa honest nikasema hajafanana na any of the two; aisee mama wa mtoto alikuwa mwekundu maana ni mweupe.

Ni kutokujiamini; watoto wadogo ni ngumu kujua wamefanana na nani; ila sababu baadhi ya wamama si waaminifu; wakisikia unasema mtoto hajafanana na baba yake wana conclude kuwa wanaonekana wezi.
 
Nasikia ikitokea mwanamke mwenye mimba akampenda sana mtu (sio kimapenzi) mtoto hufanana na huyo mtu.
 
Ngoma ni pale anapofanana na mkata majani kuanzia unyele mpaka kucha,halafu mkata majani mwenyewe yuko rafu mbaya miguu imepasuka pasuka kama magamba ya mamba vile,halafu mswaki kwake mwiko HEBU PIGA PICHA HAPO.
 
Kufanana na mwanao raha bana! Mi kuna kaka yangu amephotoa kivulana kinachofanana nae mbaya, mwenyewe huwa anajipa maujiko kweli!!
 

Huyo muuza genge lazima alikuwa akichangia kukuza mimba
 
hahaha mna kazi kweli.

Mie mwanangu binti nitaomba Mungu asifanane na baba yake! mtoto wa kike sura ya kiume iweje?
Ila kuna namna binti akifanana na babake anakuwa mzuri kweli...siwezi kuielezea vizuri lakini nimeona mara kadhaa wasichana wanafanana na baba zao halafu bado wanaonekana wazuri...ila ni kweli kuna wengine mmmh 'copy right' na baba halafu baba mwenyewe hata sio 'hendisamu'!
 
Kinababa hufurahi sana wakisikia kuwa wamefanana na baba zao, hali kadhalika nasi kina mama hufurahia kusikia watoto wetu wamefanana na Baba zao.
Hii inatujengea imani kwa wanao tuzunguka kuwa hatujachakachua

Hii kwa kweli wanayo sana kina mama/dada, unakuta mtoto labda ana siku moja au mbili tu lakini kila mdada au mama akija kumtizama...atasema amefanana na babake. Huwa inanikera hasa pale inapokuwa very clear anafanana na mamake lakini bado wadada/wamama watang'ang'ana kusema 'copy right' na babake!
 
Nasikia ikitokea mwanamke mwenye mimba akampenda sana mtu (sio kimapenzi) mtoto hufanana na huyo mtu.

Mi watoto wangu wote wa kiume na ni photocopy yangu ina maana mama yao ananipenda sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…