Baba Kisarii
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 1,844
- 3,089
Kabla hujafa tambua huu ukweli wa kila mtu anakabiliwa na shida.
Sio wewe pekee unayepitia changamoto. Hakuna mtu aliye salama kutokana na shida. Pesa, nguvu na kutembea na walinzi hakuwezi kukukinga na shida. Hata uwe na mapesa mengi shida shida itakusumbua tu.
Unapoialika shida, huwa inakubali haraka sana. Na shida ya shida ni kwamba mara nyingi huanza kama furaha. Ukweli watu wengi hawaendi kutafuta shida. Shida ina njia zake za kumpata kila mtu. Shida humpata kila mtu.
Morgan Scott Peck alianza kwa kuandika kitabu chake kilichouzwa zaidi, The Road Less Travelled, kwa maneno haya, "Maisha ni Magumu."
Pia kitabu kilichouzwa sana cha Dk. Robert Schuller kiliitwa, "Tough Times Never Last, But Tough People Do!"
Hata Yesu alisema kila siku ina shida yake (Mt 6:34).
Hata Mbaraka Mwinshehe aliimba.
🎶Shida haina ngoja ngoja.🎶
🎶Kwa maskini matajiri wote shida, shida kamwe haina taarifa huingia bila hodi.🎶
Je, wewe unasemaje kuhusu shida, haijawahi kupita na wewe?