Kila mwaka 70% ya Bajeti ya nchi inaelekezwa kwenye ununuzi, Je, thamani yake inamfikia mwananchi?

Kila mwaka 70% ya Bajeti ya nchi inaelekezwa kwenye ununuzi, Je, thamani yake inamfikia mwananchi?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Ununuzi wa umma unachukua sehemu kubwa ya matumizi ya Serikali barani Afrika, ikihusisha zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya nchi. Hii inatoa fursa kubwa lakini pia inakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwemo dosari za vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma.

Taarifa za Wakaguzi Wakuu wa nchi mbalimbali zinaonyesha kuwa kupitia mifumo ya ununuzi wa umma, kumekuwa na matatizo ambayo yamepunguza uwezo wa serikali kufanikisha maendeleo endelevu kwa wananchi.

JamiiForums kwa kushirikiana na Wajibu Institute inakuletea mjadala kupitia XSpace ya JamiiForums kuhusu Bajeti ya Tanzania na hasa bajeti inayotengwa kwa ajili ya matumizi ya Serikali. Mjadala utakuwa hewani kuanzia saa Kumi na Mbili (6:00PM) mpaka saa Mbili Usiku (8:00PM) leo Agosti 1, 2024

Wachochea Mada na Washiriki ni:

1. Dkt. Baruani Mshale: Mkurugenzi wa Mafunzo na Mikakati - Twaweza (Muongoza Mjadala)
2. Amiri Abdallah: Mshauri wa Usimamizi wa Fedha za Umma
3. Ludovick Utouh: CAG Mstaafu/Mkurugenzi Mkuu - WAJIBU Institute
4. Zitto Kabwe: Mchumi/Kiongozi wa Chama Mstaafu - ACT Wazalendo
5. Elias Chaponde: Afisa Ununuzi Mwandamizi - TRC
6. Moses Kimaro: Meneja Programu na Utafiti - WAJIBU Institute

Kushiriki mjadala kupitia XSpaces bonyeza hapa: x.com

----

Amiri Abdallah - Mshauri wa Usimamizi wa Fedha za Umma
Tunaangalia kama Mwananchi wa kawaida anapata thamani ya manunuzi yanayofanyika kwa kuwa manunuzi hufanyika kwa niaba ya nchi huku yakiwa na lengo la kuboresha huduma na miundombinu ya utoaji wa huduma hizo.

Ukiangalia ripoti za CAG zimekuwa zimeonesha tabia za kujirudia rudia za mapungufu ya katika Manunuzi, mfano Manunuzi kufanyika nje ya Bajeti au nje ya Mfumo. Manunuzi yanayofanyika nje ya mfumo ni manunuzi ambayo huitia nchi hasara

Ni manunuzi ambayo hufanyika kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011. Manunuzi ya nje ya mfumo hutufanya kununua bidhaa na huduma ambazo zipo chini ya Viwango. Matokeo ya kufanya manunuzi nje ya Mfumo ni kufanya manunuzi ambayo hayana tija. Manunuzi yaliyokosa tija kwa Taifa hayaongezi thamani kwa Wananchi.

Ripoti za Miaka Mitatu zimeonesha tunafanya manunuzi ambayo hayana tija kwa jamii. Na tuliowapa dhamana ya kufanya manunuzi wanajua kufanya manunuzi nje ya Mfumo au Bajeti ni kinyume na Sheria.

Tunapozungumza Sheria na utekelezaji ni vitu viwili tofauti, hivyohivyo katika Mifumo na utekelezaji wake. Tatizo kubwa ni ubinafsi na kukosekana kwa uadilifu, ndio changamoto ilipo.

Kuna Taasisi ambazo zina mifumo ya ndani na ni imara lakini Wasimamizi na Watekelezaji wa mifumo hiyo ni Binadamu, ambao wamekuwa wakitumia Ubinadamu wao kupindisha uhalisia, labda kwa kuwa tunaelekea katika matumizi ya Akili Mnemba (AI) inaweza kusaidia katika kuweka uwazi wa ununuzi wa matumizi ya Mifumo kama hiyo ya manunuzi.

Tunatakiwa kuwekeza katika mafunzo ya uzalendo kwa Watanzania, hakutakuwa na Rushwa wala ubadhirifu kama wale waliokabidhiwa kusimamia Mifumo ya Kimanunuzi hawatakuwa na ubinafsi na wakiwema Taifa mbele. Tunatakiwa kuondokana na ubinafsi na kuwekeza katika kuweka hofu ya Mungu kwa Watu ili kupunguza matumizi mabaya ya mifumo ya Ununuzi.


Elias Chaponde - Afisa Ununuzi Mwandamizi TRC
Mwananchi atafikiwa na thamani ya Bajeti ya Ununuzi kwa kupata huduma bora na kwa muda sahihi. Mfano: Huduma za Afya, Maji, Elimu, Barabara nk

Kama wadau wote wa Ununuzi watafuata Sheria, Kanuni, taratibu na kuzingatia maadili ya Ununuzi, lazima Mwananchi atafikiwa na thamani ya fedha ya Ununuzi. Pia, Mwananchi anaweza kushiriki katika Fursa za Ununuzi wa Umma, anaweza kushiriki kama Wafanyabiashara akipata zabuni na kuomba tenda au akipata ajira. Sio lazima kusubiria huduma zikamilike ndio tupate thamani.

Serikali kupitia Sheria wameweka fursa za Ununuzi wa Umma. Tunaweza kushiriki tukasaidia Serikali kutoa huduma, tukalipa kodi na mambo mengine yakaenda vizuri.

Tunatarajiwa Ukaguzi wa 2023/24 kutokana na uwepo wa Mfumo wa NeST kutakuwa na changamoto nyingi ikiwemo za Rushwa. Mfumo wa NeST umesaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika masuala ya ununuzi, kilichobaki hapo ni suala la uadilifu ambalo linapimwa kwa mtu mwenyewe binafsi

Mazingira hayo yatasaidia Wananchi kushiriki katika manunuzi kwa kuwa mfumo utakuwa unasaidia uwazi na kila mmoja ataamini anaweza kupata kihalali


Moses Kimaro - Meneja Programu na Utafiti WAJIBU Institute
Asilimia kubwa ya vitu tunavyoviona mfano Barabara, Ndege, SGR na mengine yote ni Manunuzi. NeST ni mfumo wa Manunuzi ambao PPRA wamekuja nao kwa ajili ya kusaidia taasisi za Serikali kufanya manunuzi kwa ubora zaidi. Na kwa kweli mfumo huo unafanya kazi vizuri.

Mfumo wa NeST ni mwarobaini wa wakati huu wa kuzuia fedha za Umma katika manunuzi ya Umma kutumika vibaya. Mfumo huu umekuja na Sheria kuwa Taasisi zote nunuzi zitumie Mfumo wa NeST au zitapigwa faini. Pia, mfumo wa NeST unabana nafasi za kufanya ubadhirifu kwamba muda wa kufanya ununuzi ukiisha mfumo 'una-block'

Mtu kama amezoea kufanya jambo fulani hata kama ni baya lakini linamfurahisha, kuna uwezekano wa mtu kuendelea kulifanya hilo jambo. Kwa hiyo hatuwezi kusema Mfumo wa NeST utazuia Ubadhirifu katika manunuzi kabisa lakini hata hivyo Mfumo wa NeST umewapa PPRA uwezo wa kuwashtaki wafanya manunuzi wanaokwenda kinyume na Sheria.


Zitto Kabwe - Mchumi/Kiongozi wa Chama Mstaafu - ACT Wazalendo
Hofu ya Mungu kwa Wananchi sidhani kama inaweza kusaidia kupunguza ubadhirifu na matumizi mabaya ya Mifumo ya Umma, tunaona kuna viongozi wengi tu wa kiimani ambao wamekuwa wakihusika katika ‘mazonge mengi tu’. Kuhusu Uzalendo, watu wengi hawajui hata tafsiri ya Uzalendo, mnaweza kuwa mnaimbishwa Uzalendo wakati upigaji unaendelea.

Ni lazima kuwe na mufumo ambayo inaongoza Mifumo ya Manunuzi, Binadamu ni ngumu kumdhibiti. Uwepo wa Mifumo utasaidia kupunguza na sio kumaliza kabisa. Mifumo inatakiwa kusomana watu wasiweze kuonana, mtu akitaka kufanya ubadhirifu apate wakati mgumu.

Tukiimarisha hizi Sheria na mifumo itapunguza ubadhirifu na kuongeza thamani ya kile ambacho kinapatikana, mfano manunuzi yanayofanyika yawe yanapatikana kihalali. Kuweka mifumo ya Check and Balance itasaidia uwajibikaji. Uwepo wa mifumo sahihi ya Uwazi na Uwajibikaji itasaidia Nchi katika manunuzi kuliko kuamini katika Uzalendo na kuingiza imani ya hofu ya Mungu.

Kuna haja ya kuwa na ufahamu kuhusu masuala ya ukaguzi katika masula ya Umma, kila Idara ya Serikali kuna “Internal Auditor” ambaye anatakiwa kufanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu

Hivyo unaweza kuwa Waziri, Mkuu wa Wilaya au kiongozi mwingine yeyote na mambo yakafanyika ndani ya Idara yako na usijue kinachoendelea kuhusu ubadhirifu

Ukaguzi wa ndani ukiwa unafanyika ndani ya mud ana kuwekwa vizuri, matumizi ya fedha yangekuwa yanaonekana kwa uwazi

Uwazi unaweza kusaidia (katika manunuzi) lakini bila kuwa na Uwajibikaji haitasaidia kama ambavyo Ripoti za CAG zinavyowekwa wazi lakini changamoto ni Uwajibikaji


Kimmito. A.K - Mdau
Wanaosema Mifumo yetu ni mizuri hawapo sahihi, Watu wengi wanaotumia wamekuwa na uwezo wa kuichezea mifumo. Nchi zilizoendelea unaweza kuiba benki ukafungwa miaka miwili lakini ukiiba fedha ndogo tu ya Serikali madhara yake ni makubwa na adhabu yake inakuwa kubwa.

Hivi inakuwaje kuna Polisi, Waziri na viongozi wengine wengi hawaoni tatizo lakini CAG akienda kwenye Taasisi wiki mbili tu anabaini madudu, hao wengine hawakuona?


TONY ALFRED K - Mdau
Ni mara chache kuona Taifa likipiga hatua kwa msukumo wa ndani sisi wennyewe lakini mara nyingi tumekuwa tukipata msukumo kutoka nje ya Nchi mfano kutok IMF, WHO na wengineo. Kuendelea kutegemea msukumo uwe unatokea nje hiyo inaonesha sisi hatukui.

Kinachofanyika ni kama hatujitendei haki na ni kama hatukui, mfano PPRA walikuwa wanatoa ripoti yao kila Mwaka, cha kushangaza mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2023, wanasema Ripoti yao inaenda kwa Rais, na akiamua kupelekea sehemu nyingine kama Bungeni ni kwa maamuzi yake wakati miaka ya nyuma ilikuwa inatolewa hadharani.

NeST ni mfumo mzuri tofauti na ule uliopita ambao ulikuwa unasimamiwa na Watu wengine, mfumo huu wa sasa una vitu vizuri. Lakini tumekuwa tukioneshwa katika hatua za awali, hatua za matumizi ya Mtandao zinazofuata haziwekwi wazi, hivyohivyo ndivyo ilivyo katika masuala ya Mikataba haiwekwi wazi.

Kuna kasumba mbaya Nchini kuwa Fedha za Umma hazina mwenyewe, hiyo imechangia Watu wengi kuwa na nia ya kutaka kuzitumia vibaya.


Zesane JR - Mdau
Watu wanapigia kelele masuala ya Sheria lakini zinapokuwa zinashughulikia masuala husika zimekuwa hazina ukomo na hazina ‘impact’, mfano Ripoti za CAG zinasomwa hadharani na ubadhirifu unawekwa wazi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, watu wanaona zikisomwa hawaoni Uwajibikaji.

Kukosa Uadilifu kuna wakati unaweza kusababishwa na maslahi duni, inawezekana Watu hawapati maslahi mazuri yanayoendana na uhalisia wa Maisha, hivyo anapopata nafasi ya kufanya ubadhirifu anafanya hivyo.

Watumishi wa Umma wawe na uchungu na rasilimali za Wananchi, kwani asilimia kubwa rasilimali nyingi zinapotea mikononi mwao


Ezy_daboss - Mdau
Ununuzi umekuwa ukiathiriwa na presha kutoka kwa Wanasiasa, pia Mnunuzi hana kinga inapotokea anataka kupingana hoja na Mwanasiasa ambaye anaweza kuwa na nguvu y kushawishi mabadiliko ya mchakato

Kuna haja ya hali hiyo kuangaliwa jinsi ya kudhibiti au kubadilisha mazingira ya aina hiyo
 
Hivi kwanini hii mijadala isingekuwa inaletwa humu humu JF.
Hii itasaidia kufatiliwa zaidi kwa jukwaa hili na kuweza kuvutia watanzania wengi kujiunga na jukwaa hili.
 
Pongezi nyingi sana kwa walio liona hili,Mungu awatangulie.

Naomba Mjadala mwingine ujikite hapa,

MAPATO YA NDANI vs DENI LA TAIFA

Deni lililopo na gharama za ku Hudumia deni hilo.
 
Back
Top Bottom