Kila mwaka, March-April...

Roulette

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
5,568
Reaction score
5,386
Hi all,

Kwa mwaka wa tatu sasa nimenote kua I develop a strong insomnia that impacts severely on my ability to focus, to work, to interact socially and just to be useful to myself and people around me (Rejea thread hii). Na insomnia hiyo inafika to its worse around march-april. This time I am on leave for a month, so kazini it is fine, but socially it is a disaster, natamani nijifungie tu ndani hadi nitakapo rudi to mynormal self.

I am a bit worried, I am now trying to remember tatizo hili lilianza lini hasa. Sijui kama I had this problem in 2010, 2009 and years before. I know I had sleep problems but I never noted the months. Pia najaribu kujiuliza why March-April? Is it just a coincidence or is there something preventing me from sleeping around these months?

Kuna advice nilipewa humu humu JF ambazo zilisaidia, but zinasaidia only toward mid-april, tarehe ambapo ni vigumu kujua kama tatizo limeisha lenyewe au limeisha kwa sababu nimefata ushahuri. I have also been advised to consult a medical doctor who will help me identify the causes and eventually cure this problem once and for all.

I just felt like sharing again this problem. It is 1am na sina hata tone la usingizi, my man is sleeping, all my friends mtandaoni too. I will just read a book or write a little as I wait for the early morning to come. Sometimes napata usingizi for an hour or two ila bahati mbaya kesho I start my daay at 5:30 am. Usiku mwema kwa wanao lala, you don't know how lucky you are.
 
Very sorry for you,...dont worry I am here for you at least to chart with you till dawn when your hubby is awaken... I was created for those with problems like yours...
 
Pole Roulette for some reason i'm still awake too and i just read that FFI stuff scary uh.....
Maybe a psychologist would be of much help
 
Last edited by a moderator:
Seriously smoke weed the problem will not exist am assuring you, before it was declared illegal it was used as a medicine to babies and grown ups who had insomnia, you can even google and see for yoself. it is not harmful as they claim it is.
try that and u'll find me unishkuru u'll see.
Goodnight
 

Dada pole sana. Mimi sio daktari wa sindano (medical doctor) lakini nimekula chunvi nyingi na matatizo kama hayo nimeyakabili kupitia ndugu zangu na mahbub wangu pia. Matatizo haya ni common kwa watu walioko northern hemisphere. Wewe sijui uko wapi?

Hizi hapa ni njia mbili watu wangu wa karibu walizofanya kutatua tatizo lako:

1. Fanya mazoezi ya nguvu jioni (uchoke). Hii itasaidia kukupa usingizi.

2. Tumia dawa hii "DIPHENHYDRAMINE HCL 50mg" Hii ni off-the-counter sleep aid medication ambayo sio habit-forming. Utalala kama pono dada. (note: unaweza kuanza na 25mg uone kali yake. 50 mg ni maximum strength. Muulize mfamasia wako hii dawa.) Mimi huwa naitumia sana hii dawa ninapopata shida ya usingizi.

Bado ni muhimu umuone daktari kwa ushauri wa kina.

Kwa wale medical doctors humu jamvini, tafadhalini msaidieni huyu dada. Tatizo la kukosa usingizi ni kubwa na hulijui ukubwa wake mpaka likikufika. Please help!!
 
Pole sana mamito.
Kama inatokea wakati uko likizo, maybe you dont get tired enough? or else you become too tired (siwezi kulala nikiwa nimechoka sana). Gym inaweza kukusaidia sana ama swimming for that matter. Lakini excitement ama kuwa anxious kunaweza kukuzuia kulala pia. Try to calm down and take a shower just before bed. A comic movie onbed ( dont know how healthy that is) might help too.
Otherwise inabidi uje mie na Paw tukufanyie unasihi, lol
 
UKOSEFU WA USINGIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.
Madhara ya ukosefu usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalan, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine yafutayo:

HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA MOYO

Unapokosa usingizi, mfumo wa uzalishaji homoni huvurugika ambapo uzalishaji wa homoni za ‘stresi'
(stress hormones) huongezeka. Pia husababisha vidonda vya tumbo na hali ya kusikia njaa hata kama umetoka kula muda mfupi. Uko hatarini kusumbumbuliwa na hasira na ghadhabu kila mara.

ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU

Ukosefu wa usingizi huchangia pia ongezeko la shinikizo la damu, pia huchangia kuzeeka kwa mtu kutokana na kuvurugika kwa uzalishaji wa homoni za ongezeko la umri. Humfanya mtu kuonekana mzee ili hali bado ana umri mdogo.


KUZIDISHA TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO

Ukosefu wa usingizi huchangia pia tatizo la ukosefu wa choo na huweza hata kusababisha kifo kama tatizo likiwa sugu.


EPUKA KUTUMIA DAWA ZA USINGIZI

Kama unasumbuliwa na tatizo la ukosefu wa usingizi, jua kwamba hauko peke yako. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Taasisi ya Taifa ya Usingizi
(National Sleep Foundation –NSF), umegundua kuwa kati ya watu 10, ni wanne tu hupata usingizi mzuri kila wiki.
Pamoja na kuonekana kwa athari nyingi za kukosekana kwa usingizi, lakini utakuwa unajiweka katika madhara na hatari zaidi iwapo utalazimisha kupata usingizi kwa kumeza dawa za usingizi, kwa sababu ni hatari na mara nyingi dawa hizo huwa hazisaidii kuondoa tatizo.


JINSI YA KUFANYA ILI UPATE USINGIZI

Kwa asili yake, kichocheo cha usingizi mwilini kijulikanacho kama ‘melatonin' hupatikana kwa ulaji wa mboga za majani na matunda mbalimbali ya kuongeza virutubisho mwilini na hupatikana pia kwa kupata mwanga wa jua wa kutosha wakati wa mchana. Hivyo huna haja ya kumeza vidonge badala yake zingatia uzalishaji wa kirutubisho hicho kwa mlo na mwanga wa jua.

Ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata usingizi mzuri, unashauriwa kuepuka kufanya yafuatayo muda mfupi kabla ya kupanda kitandani kulala:

Epuka kuangalia TV au kompyuta muda mfupi au saa moja kabla ya kulala, kwani teknolojia hizi siyo nzuri sana kwa macho kutokana na mwanga wake, hasa kwa mtu mwenye matatizo ya kupata usingizi.

Epuka kulala huku taa inawaka, hakikisha unalala huku taa zote zikiwa zimezimwa, licha ya mwanga wa taa usiku kusababisha madhara mengine, lakini huchangia kuharibu mtiririko wa usingizi. Hata uamkapo usiku kwenda msalani, ikiwezekana usiwashe taa ili kuepuka kuvuruga usingizi wako.

Usilale karibu na vifaa vya umeme na vyenye sumaku kama vile saa, simu, au redio kwani huchangia kudhoofisha uzalishaji wa homoni za usingizi. Hata saa yako yenye ‘alarm' ya kukuamsha, unashauriwa kuiweka mbali nawe kabisa.


Mwisho, hakikisha unakuwa na ratiba ya kulala inayoeleweka na hakikisha unalala muda huohuo kila siku. Kwa kawaida mtu anatakiwa kulala kati ya saa tatu na saa nne usiku. Iwapo utazingatia vyote vilivyoelezwa hapo juu, bila shaka utaweza sasa kulala usingizi mnono.
 
Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA1
. KUTOPATA USINGIZI

Chukua kijiko kimoja(10ml) cha unga wa habat sufa,changanya na glasi 1(250ml) ya maziwa .Kunywa na rudia kutumia kutwa mara tatu kwa muda wa siku saba.

TIBA 2
. KUTOPATA USINGIZI

Chukua kijiko kimoja cha unga wa habat saudaa,changanya na kikombe kimoja(200ml) cha maziwa moto.Changanya na asali halafu soma dua ifuatayo
اللهم غارت النجوم و هدأت العيون و انت حى قيوم لاتأخذك سنة ولا نوم يا قيوم أهدء ليالى وأنم عيونى
Utasoma dua hiyo mara saba na kisha utakunywa dawa hiyo.Utalala.

TIBA 3: KUTOPATA USINGIZI

Changanya kijiko kimoja (10ml) cha unga wa habasoda na vijiko(10ml) viwili vya asali ndani ya glasi(250ml) moja ya maziwa moto.Kunywa usiku kabla ya muda wa kulala. Mkuu.@Roulette Tumia hizo Dawa kisha uje unipe Feedback.

Chanzo:MziziMkavu
 
Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia miguu katika maji ya Uvuguvugu .

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunywa maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6. Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.
 
What is your geographical position? (uko nchi/upande gani wa dunia)? Kama hauko Bongo, winter season inaanza lini mpaka lini?
 
Pole sana mm mwanzoni nilijua usingizi au kulala hakuna effect yoyoye,lakin baada ya kwenda jeshini ndipo nilijua faida ya usingizi,kwani baadhi ya watu walikiwa wanachanganyikiwa kabisa anakuwa kama Kichaa,Nadawa ilikuwa ni kulala zaidi ya Masaa 12 ndo unarudi katika hali ya kawaida,Mimi nakushauri jitahidi kufanya Mazoezi na kufuata ushauri wa Dr Mzizi mkavu.na Mungu wetu wa upendo atakusaidia

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Very sorry for you,...dont worry I am here for you at least to chart with you till dawn when your hubby is awaken... I was created for those with problems like yours...

Asante but sihitaji msaada wa kuchat
 
What is your geographical position? (uko nchi/upande gani wa dunia)? Kama hauko Bongo, winter season inaanza lini mpaka lini?

Nipo EAC, nasafiri safiri humu humu, except mwaka jana ambapo tarehe hizo ziliambatana na winter nilukokua.
 
Pole Roulette for some reason i'm still awake too and i just read that FFI stuff scary uh.....
Maybe a psychologist would be of much help

Asante Lizzy. Nitaonana kwanza na generalist. Jana baada ya kurusha hii thread nilizama kwenye yoga na meditations fupi fupi, nikaja pata usingizi arnd 3
 
Last edited by a moderator:

Been there, it helps but doesn't solve the problem. Useful for extreme days lakini.
 

Asante sana. Kuna pills natumia sometimes zinassidia, sometimes hazisaidii. Nipo Bongo so we can't blame it on the location...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…