1. Wewe sio mgeni huku jamvini. wageni wote wanabisha hodi
2. Wewe sio mchanga kwenye mambo ya mapenzi....kitendo cha kufikia una mtoto umefuzu kwenye mambo ya kikubwa...age aint nothing..
3. Una matatizo kisaikolojia...unahitaji kuonana na wataalamu wa saikolojia watakushauri vizuri endapo utakuwa mkweli na kuweka wazi matatizo yako....huenda unajiona wewe ni mzuri mno, ubinafsi au dharau na kutochukulia relationship serious issue.
Huna upendo wa kweli na wa dhati kwa hao wanaume unaobahatika kuwa nao. unajenga uhusiano kwa maslahi tofauti au kwa sababu tuu basi mwanamke anatakiwa awe na boyfriend au mwanaume awe boyfriend kama fashion.
Baada ya kusema hayo basi ningependa kuchukua nafasi hii kukushauri kwamba chukulia wanaume wote ni sawa..usijali kipato, elimu au sura. Angalia busara na hekima za mtu na upendo wa dhati. Usichukulie mzaha mzaha inapofikia issue ya mahusiano. badili mwenendo ondoa hisia hasi juu ya wanaume na utafanikiwa kuwa na uhusiano wa muda mrefu au hata wa maisha na mwanaume utakayempenda kwa dhati.