Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

Pole ndugu. Huyu mwanamke ulimchukulia wapi? Amelelewa katika mazingira gani? Kabila Gan? Dini? Funguka tuponye vijana wanaopenda kuoa bila kuchunguza tupone


Duuu, haya bwana ndoja tu nifunguke. Originally ni watu wa kigoma (Wamanyema) ila yeye kazaliwa tanga maana maisha ya wazazi wao kwa muda mrefu wameishi tanga, baba yao alikuwa driver wa bus, ila nahisi kuna mzazi Mmoja ana asili ya kitusi maana hata yeye ana sura ya kitusi kwa mbali.

Hata msichana Wetu wa kazi wakati huo alikuwaga namfananisha na demu Mmoja wa ile kwaya ya Rwanda Ambassadors of Christ sijui, walioimba "kwetu pazuri"

Mama yake mpole sana sana, ila sijui labda kwa vile sijawai kaa naye sana ila hata kwa muonekano ni mpole sana. Hata huyo mwanamke kimuonekano ni mpole.

Dini ni mkatoliki, ila mimi ni mlutheri na baada ya kuanza kuishi pamoja alikuwa anasali Lutheran.

Walipokuwa wanaishi sio uswahilini, baba yake alifariki akiwa bado Mdogo, na yeye walizaliwa mapacha ila Bahati mbaya Pacha mwenzake alifariki.

Inatosha nadhani mkuu
 
🤣🤣🤣🤣🤣Asante mkuu, hapana mkuu niliachana nako, maana kwa yale mapito sometimes hata hata network ilikuwa haishiki,,,you know what I mean🤣🤣🤣🤣🤣

Nimekuelewa mkuu, Mungu akujalie uzee wenye furaha maana sarakasi za ujana hazikua za kitoto🤣🤣
 
Umegundua Nini ilikuwa mchango wako katika kusambaratika kwa familia yako?


Mkuu nilikosea nikaomba msamaha mwenzangu akaniambia yameisha, zaidi ya yote hata baada ya yeye kuuza vitu nilijaribu Kufanya kila nililohisi litasadia yeye kurudi na tuendelee na maisha ila mwenzangu akakataa.

Nahisi baada ya kuuza vile vitu na kupata hela alidhani maisha ameyapatia ndo maana alikuwa anamjibu kila mtu shit.

Ila Mkuu trust me nilifanya bidii Zote z kumrudisha ila ikashindikana. Sasa sijui ningefanyeje zaidi ya hapo.
 
Una mambo mengi ya kufanya.
Achana na watu walioshindwa maisha. Fanya yako mkuu
 
Kweli ulijitahidi.ba
Nimefurahi japo sio vya kufurahi tatizo nipo mji tofauti na yy na nimtumishi japo ni shirika binafsi
Basi ukijitahidi. hakukuwa na namna lakini wanaume Mara nyingi huwa ndio tunaoanza kuvuruga familia
 
Msamehe tu huyo mpuuzi ila usikubali kurudiana naye kimahusiano/mke & mume.
Yuko mpuuzi mwenzie alinifanyia ya hovyo kabisa mara kibao,usaliti mpaka kupata maambukizi ya HIV lakini nikamsamehe,baada ya kumsamehe bado akaendelea na ushenzi wake,nilimbwaga ila nimemsamehe
 
Samehe saba mara sabini, pia anapokwama msaidie kumbuka ndio mama wa wanao huyo akifariki huzuni kwa wanao so usimbeze

Majaribu hayakwepeki na wewe ndio lilikuwa jaribu lako.
 
Samehe ili uwe huru nafsini mwako japo usimrudie tena
 

Waliopitia changamoto ngumu za ndoa tuu ndio wanaweza kukuelewa.
Hakuna ndoa ngumu kama ya kuishi na mtu sababu ya watoto au sababu ya cheti cha ndoa. Unaweza kufa ukiwa unajiona hivihivi
 
Amina asipo kuelewa basi tena ata kuwaona watoto sio kitu Kibaya ili mradi afanye kwa tahadhari
 
Pole Bro. Huyo Mama mkwe vp kazeeka sana? Shape vP?. Ingekuwa mm ningemuomba ili nilipie y'all mabati na 1m ya kununulia shamba
 
Aisee, wanaume tunapitia magumu sana, pole brother ila kwa story hii, someone else has to learn what comes from really love. Shukuuru tu Mungu kwamba aliamua kufanya hivo mapema, imagine if you had had accumulated alot of wealth ndio akaamua kufanya hivo..or the most she could kill you to give her space to dominate the territory. Thank God and forget all about that
 
Duuuuuhhhh haya mambo ya familia haya, kuna ulazima mkubwa sana wa wazazi au viongozi wa dini hata na serikali waliangalie hili suala kwa ukaribu zaidi, maana siku hizi kwakweli ni balaa, na kwa hali hii mauaji ya kimapenzi iwe ndoa au wanaishi pamoja tu au wamezaa tu hayataisha kwakweli. Dunia hii basi tu, huyo mwanamke nadhani kuna mda anakumbuka sana maisha yale anajuta sana ila ndo hivyo maji yakimwagika. Hili liwe fundisho kwetu sote wanawake na wanaume pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…