Kila Nikikumbuka Hili Tukio Huwa Nakubali kuna watu wana Akili sana!

Alfred

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2008
Posts
2,093
Reaction score
2,843
Nikiwa Mwaka wa Pili pale udsm mwanangu mmoja alikuwa akisoma dit, alikuja kuchukua michoro yake kwangu pale udsm (Autocad drawings za Civil), baada ya kutoka pale akaenda kwa bro ake (alikuwa na pc) kwa maelezo yake alienda geto la bro ake kuchukua pc ya bro na kuipeleka kariakoo kwa bro!

Mwana baada ya kutoka kwa bro ake, akapanda daladala pale mawasiliano, akiwa nabegi lake sasa lina pc mbili ambazo zina thamani ya karibia M2.5, ile kupanda daladala akaguswa bega akaambiwa niaje kaka, fresh fresh!

Mshikaji aliyemgusa bega alikuwa ni rika lake tu, akamuuliza kwa unyenyekevu kinoma bro unaweza kunionyesha BUREAU DE CHANGE Maeneo haya ya karibu, mshikaji akasema yeye hajui, huyo mshikaji akambembeleza akamwambia nisaidie kaka yangu hapa nina pesa nyingi (dola) nataka nizichange then nieke banki ila naogopa kutembea umbali mtefu naogopa kukabwa (hapa anafumua bag kuonesha madola)!

Mwana akakaza kwamba bwana yeye bureau de change hazijui maeneo ya mawasiliano, mara mzee mmoja anaingilia mazungumzo yao, anawauliza na kijana wa madola anamjbu shida yake.. mzee akawaambia msihangaike bureau de change iko hapa nyuma tu mawasiliano.. mwanangu akamwambia huyo mshikaji nenda na mzee huyo ushapata msaada tayari.. Mara yule mzee akamwambia mshikaji wangu, Hapana msindikize rafiki yako mimi nimewakuta wote msitengane.. na mwana wa madola akamwambia mshikaji wangu amsindikize na akamtoa 30K ya usumbufu.. Mwana akakubali bhana!

ile wamefika bureau de change (Kumbuka bado mwanangu ana bag lake mgongoni).. mwana wa madola anamwambia sasa mwanangu wewe ndio mjanja hapa naomba tusaidie kuchange, kwa kuanzia akampa dola 100 akajaribu kwanza, mwanangu akaenda akiwa na bag lake mgongoni.. Pesa zilichenjiwa akapata laki mbili na ushee..

Alivorudi kuwapa feedback, akawapa ile laki mbili na chenji alizopata baada ya kubadili.. kisha wakamwambia sasa chukua hizi zilizobaki ukachange sisi tutakupa milion 5 na tuzime simu zetu tusije tukavamiwa maana hizo pesa ni nyingi sanaa zaidi ya M100, weeh dogo akakubali bhana M5 kwa mwanafunzi ni nyingii saana.. na akawa anajiamini si ameshatest zile dola 100 zimekubali?.. kisha wakamwambia acha simu na bag lako na vifaa ambavyo unaweza fanya navyo mawasiliano.. mwanangu akafanya Hivyo! na kwakuwa walikuwa wanafanya hivyo mbele ya bureau de change office na yule customer care alikuwa akiwaona.

Mwanangu akapewa bag lenye madola, akaingia ndani kupokea mamilioni.. customer care akazichukua akazitia kwenye Mashine...Aisee Mashine ilizitoboa zile dola zote.. kumbe zilikuwa feki asee.. Mhudumu akacheka saana.. akamwambia dogo ushapigwa!

Anakimbia Nje kuwaangalia washikaji.. Hata unyayo hakuukuta!

Alfred
 
Huyo aliepigwa kizembe alikua anatokea Chatu enzi hizo.....
Leo hii ndio amekua m-babe na Amiri # 1 nchini, na kwakua anaishi pale ukingoni mwa ferry, basi ameamua kulipiza kisasi kwa wale wote "janja" pamoja kuhakikisha Jitu na Malila hawachomoki....tehteehh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…