Skillionare
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 1,190
- 526
Wakuu kila nikipika wali bado hautoki vizuri ,nipeni ujanja wali utoke mmoja mmoja,sababu nikuandalia wali unaweza usitofautishe na ugali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ratio ya maji na mchele ni muhimu sana.
Unatakiwa kutumia 1:1.5 (mchele:maji). Hakikisha umefunika na umeweka kila kinachitakiwa. Usifunue funue wala kugeuzageuza. Hakikisha moto sio mkali bali wa wastani.
Utashangaa matokeo super just like in a rice cooker.
Kama huwezi kufanya hivyo pata/nunua rice cooker but it works the same.
Inawezekana unaloweka mchele halafu wakati wa kupika bado unajaza maji kana kwamba mchele ni mkavu sana........Angalizo lingine, kama mchele ni mpya nao unawasumbua wengi, kwani kimsingi unakuwa ni kama ambao ulilowekwa, kwa hiyo mapishi yake ni muhimu maji yakalingana na mchele (vikiwa jikoni). Kwani maji yakiwa mengi, huo wali wako utatota (utakuwa kama ugali)...
Njoo unipikieKupika wali kumbe ni mtihani kwa wengine....
Njoo unipikie
Endelea tu kula ubwabwa wako......haji mtu :becky:
Itabd nile pepeta. Unaujua?
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
nakumbuka mama wakati ananifundisha jinsi ya kupika wali wa nazi kipindi hicho alikuwa akinieleza ipo siku utakuwa peke yako nakumbuka nilikuwa na miaka 12. siku ya kwanza akanifundisha kuondoa mawe kwa kutumia maji siku ya pili na kisha kupika wali nakumbuka alikuwa akisema utamu wa wali mahaba ndio yakuonja kujua wali imtamu kiasi gani halafu akachukua ukoko wa chini akaniambia nile kama nikikuta kokoto au mchanga atanipa 200/= sikukuta mchanga wala kokoto akaniambia kesho yake nikanunue sufurua ndogo nipike na nikiupika vizuri basi atanipa 500/= nikanunue nitakacho kwakweli alitumia technic ya zawadi kunifundisha na kwakweli kama alijua kuwa kuna kipindi nitaisha mwenyewe mbali na nyumbani na miaka kadhaa kabla ya kuoa.
Nakumbuka alikuwa akinieleza kuna wali waweza kuwa
1. wa kiini cha 1 au 2
2. uliotota
3. bokoboko
4. uji
Ahsante sana mama ulivyokuwa unanifundisha bibi alikuwa akikulalamikia kuwa unanitesa kwa kunifanya nipike na kama sio ukali wako nisingejua kupika vyakula mbalimbali hii inanifanya wakati mwingine kumsaidia mke wangu kupika siku za weekend au nikimuona kachoka kwasababu ya kulea mtoto na kipindi chake cha ujauzito. Ni wewe mama uliyenifundisha kuwa hakuna kazi ya mwanamke kwani nilikuwa mtoto pekee wa kiume na sikuwa na dada au kaka kwa sasa naweza pika chochote nitakacho kuanzia pilau biriani vibibi hadi mikate karibia yote tupendayo kula kuunga kwa nazi au kwa mafuta. Ahasante mama ijapokuwa leo unatimiza miaka 17 tangu ututoke hakika najivunia kuwa na mama kama wewe nakupenda sana na Mungu akulaze pema peponi wewe pamoja na Baba sintoisahau ajali ile iliyoondoa roho zenu nami kupona kwa miujiza
Wali ili utoke umenyooka kwanza kaanga mchele uliooshwa, kulowekwa dk chache na kuchujwa maji kwa kuutia kwenye mafuta ya motoo (vijiko vikubwa 2 vinatosha ubwabwa wa watu 2, manake najua kiporo kina sehemu yake,lol). Geuza kama dk 1 tu, kisha tia maji ya moto kiasi cha kufunika mchele wote tu na sio zaidi. My moms recipe ilikuwa kikombe cha mchele kwa kikombe unusu kwa maji japo siitumii hiyo. Mchele ukianza kuchemka tu punguza moto na hakikisha umefunika sufuria. Usigeuze hadi maji yakauke. Geuza na angalia kama una kiini. Unaweza kumalizia kwa kuweka kwenye oven ama kupalia mkaa.
Tip: kubadilisha ladha ya ubwabwa wako unaweza kuweka:
1 binzari nyembamba aka jeera kiduchu.
2 Baada ya ubwabwa kukauka maji unaweza kuweka a grated onion kabla ya kugeuza. Ladha yake utaomba poo.
3 Well, kichaa kikikushika a pinch of binzari sio mbaya.
hiyo rice cooker itabidi niitafute asante mkuu