Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Maendeleo ya Mpira wa miguu pamoja na michezo mingine inategemea sana uwepo wa viwanja,tena vilivyo bora. Nasoma historia kuwa baada ya kuja kwa vyama vyingi vya siasa CCM walijimilikisha vyanzo vingi vya uchumi ikiwemo viwanja wa michezo, vilivyokuwa vinamilikiwa na serikali chini ya chama kimoja. Sjui kwanini waliamua hivo ila kwangu bora wangejimilikisha mali zingine zote ila wangetuachia viwanja vya michezo. Kwa ufupi hivi viwanja vimetelekezwa. Mwaka 1995 niliingia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora,kwakua nilikua mdogo sikujua kama bado haukuwa umekamilika ila nilikuja kujua baadae. Uwanja huu ulijengwa miaka ya 1985 haujakamilika hadi leo. Sizani uwanja huu usingekamilika hadi leo kama ungekua unamilikiwa na serikali lazima kuna kitu kingefanyika. Viwanja km cha Sokoine Mbeya vinatia aibu mno.Kiwanja kimechaa utazani banda la ng'ombe. Hata tukiwa tunaangalia kwenye TV ni aibu tupu! Pitch ndo usiseme viwanja km majaruba ya mipunga. Mifano ya viwanja vibovu vya CCM ni mingi wadau mnavijua.CCM kwa nia nzuri tu ya michezo ya nchi hii hasa mpira wa miguu rudisheni hivo viwanja serikalini ili vitengewe bajeti vikarabatiwe tutawaona mna tupenda sisi wapiga kura wenu,maana hata serikali ni yenu kwani shida iko wapiiii? Sote tunaona jinsi ajira za maofisini na viwandani zilivyongumu.Tunahitaji vijana wengi wajiajiri kwenye michezo lakini ni lazma serikali iwavutie vijana kwa kuboresha miundombinu hasa viwanja. Km hamuwezi kuvikabidhi serikalini basi ingieni ubia na wadau wa michezo Mfano TFF ili waviboreshe mtuondolee hii kero ya ubovu na uchakavu wa kutisha wa viwanja. Natumai ombi langu litatekelezwa michezo ni kiwanda!!!!!!