Kila ninaposaidia mtu, narudishiwa jeuri

Hongera kwa msaada unaonekana una roho ya huruma sana,
Endelea hivyo hivyo rafiki!
 
Mie mtu ananiomba hela hajala na hajui ale Nini,natoa kiakiba changu nampa.kesho nasikia kauza Mali kapata millions hanikumbuki hata Kwa buku mbovu.
Mi nalala njaa sikumbukwi
Mtu mpaka anauza Mali zake maana yake shida na matatizo yamemfika hapa.

Usimlaumu sana.
Pengine Hela zote amelipa madeni.
Ukimsaidia mtu, Fanya kama hiyo Hela imedondoka umeipoteza.

Msaidie mtu kile ambacho unaona unao uwezo wa kukitoa bila kukuletea shida,
usitoe kitu halafu nafsi Yako baadae ianze kujutia Kwa namna yoyote
 
Sister Abigail Inatakiwa uchange mindset yako haraka sana sio vizuri kuwa na Mawazo ya namna hiyo.

Tambua kwamba ulichokuwa unatoa au kusaidia sio deni balii ni msaada, ukiendelea kufanya misaada unayotoa kutaka kumfunga mtu sio jambo zuri ni bora usisaidie.

Kama kweli umeguswa na tatizo la mtu na unaweza kusaidia basi saidia na usitegemee return yoyote au favor yoyote kutoka kwa huyo mtu.

Watu kama wewe now mpo wengi kwenye society yaani unakuta mtu kila siku ni kulalamika mala wale watoto mimi ndio niliwasomesha lakini now hawanikumbuki. Nilimtafutia kazi lakini amegoma kumuunganisha mtoto wangu, Amepata kazi lakini hakumbuki kunitumia pesa etc etc

Please please please Usifanye wale uliowasaidia kuwa mateka wako, kwamba ukitaka chochote kutoka kwao na wewe wakusaidie saidia halafu upite kushoto.

Kuna jamaa yangu baada ya kuunganishwa kazi ya jeshi toka 2013 hadi leo amekuwa mtumwa wa aliemsaidia. Kuna Dada yangu wa kwanza alisomeshwa na ndugu yetu baada ya kupata kazi amekuwa mtumwa na maneno anakopwa hadi mi5 .kuna Mwingine alisomeshwa na Mjomba wake now amekuwa mtumwa.

Kuna lile kundi ambalo huwa unakuta mtu anasema mimi ndio nilikuwa bora nawasaidia hata kwenye masomo lakini wana wametoboa hawanikumbuki zinaanza lawama huo ni ujinga.
Tusipende kusaidia baadae tukaanza kusema na kusengenya watu dunia imebadilika watu wanapitia changamoto nyingi.
Kama umepata opportunity fulani ya kutoboa kwenye Maisha kamwe usije ukamuachia mtu hata kama ni ndugu wa tumbo moja, Baadae uje uanze kulalamika ile ilikuwa ni nafasi yangu nilimuachia Akatoboa ila sasa anisaidii.
Please please please narudia tena kama huna moyo wa kusaidia ukasahau Ni bora usisaidie kuepeusha lawama zisizo na msingi.
 
Mimi maswala ya kusaidiana sinaga kabisa.

Nilishasaidia watu, halafu wakaingia mitini.

Sasa naishi kama mjerumani, nakufa na tai shingoni.

Sisaiidi mtu na wala sihitaji kusaidiwa.

Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
 
Nadhani hujanielewa.
Siweki matarajio
Na sijui kwako because nlikusaidia.bali nakuja kwako because we ni ndugu kwangu,kaka dada etc
Hiyo nlosema no kama reference tu why unamuonyesha mtu upendo lakini yeye anakuwa wa baridi kwako?
 
Sitegemeagi kitu kamwe.
Bali nawafuata kama wapendwa wangu pale nnapokwama.
Kama watu wa karibu sana
Nkiwa na Imani ntasaifika kwao
Achana na kusaidia watu.

Punguza wema binadamu hawana kumbukumbu.

Kila mtu auchukue mzigo wake mwenyewe.

Hii Dunia kila mtu alikuja mwenyewe na ataondoka mwenyewe.

Kila mtu ajitwike msalaba wake mwenyewe.

Akishindwa akafie mbele.

This world is not for the weak.
 
Nadhani hujanielewa.
Siweki matarajio
Na sijui kwako because nlikusaidia.bali nakuja kwako because we ni ndugu kwangu,kaka dada etc
Hiyo nlosema no kama reference tu why unamuonyesha mtu upendo lakini yeye anakuwa wa baridi kwako?
Nimekuelewa vizuri kabisa . Ndio maana nikasema Ondoa matarajio kabisa hata kama ni ndugu wa karibu
Wewe huoni inafika mahala mtu pamoja na kulelewa na wazazi wake ila inafika muda wazazi wamezeeka bado wanak
Vipi kuhusu hao ndugunwengine
 
Tunahitajiana Kwa nionavyo.
Ila sawa nimejifunza
 
Nimekuelewa vizuri kabisa . Ndio maana nikasema Ondoa matarajio kabisa hata kama ni ndugu wa karibu
Wewe huoni inafika mahala mtu pamoja na kulelewa na wazazi wake ila inafika muda wazazi wamezeeka bado wanak
Vipi kuhusu hao ndugunwengine
Sawa mkuu
Ntapambana na Hali yangu😊
 
Mimi kiukweli moyo wa kusaidia sina kila nikiwaza kusaidia moyo unaniuma siku nzima hivyo nimeamua kutokuumiza moyo wangu japokuwa vya kusaidia vyenyewe sina ila hata sijui buku ,sijui nimnunulie mtu pombe basi jua nitaumia moyo siku nzima hivyo mimi sisaidii wala siombi msaada nakufa na maisha yangu
 
Sawa mkuu
Ntapambana na Hali yangu😊
Tanzania tunaendeshwa na mifumo ya kijamaa. Tunaishi kwa kusaidiana ,Ukikwama unaomba tu msaada lakini haina guarantee kwamba utapata kama wewe unavyotoa.
Ndio maana hata wewe ukiwa unatoa msaada inatakiwa utoe kimkakati sana.
Mimi nilishachange mindset yangu kabisa sitegemei msaada wa mtu. Nilikuwa na marafiki kibao bata nyingi lakini nilivyoanguka .nilijikuta nimebaki mimi peke yangu geto, hata kodi nilikoswa. Baada ya hapo nilijifunza self reliance.
Na hata nikisaidia mtu tatizo kubwa yaani sitegemei fadhila zozote kutoka kwake . Msaada unaweza pata tu kwa stranger ambe hata huna mahusiano nae.
 
Sawa boss..nimeelewa
 
Yalikukuta yapi Hadi uwe hivo?
 
Wewe ndiye mwenye shida, kujiweka karibu na watu unaonekana unajipendekeza, ishi maisha yako wewe kama wewe ufaidi mema ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…