Hahaha wanakopa kwa niaba yako.
Kinachonichosha mimi, kwanini wanapokopa huwa hawatuambii, kwamba wanataka kukopa kiasi fulani kwa fulani kwa masharti haya, na riba itakuwa kiasi fulani, na tunataka pesa hizo kwa ajili ya kufanya , kazi A,B, na C.
Masharti ya mopo tunatakiwa kulipa deni baada ya muda fulani, na tusipolipa ndani ya muda huo tutakumbwa na tatizo A,B na C.
Wao wanakopa kimya kimya , huku kwenye majukwaa wanatuambia ni pesa za ndani, miradi tunasikia mara imefadhiliwa na Bank ya Dunia mara, Serikali ya Japan , mara Finland, wao wantuambia Mama A anajenga, anfanya hiki, hili huwa lina nichanganya sana, hakuna uwazi wowote.
Lakini sasa tizama mabilioni yanayolipwa, hatuambiwi analipwa nani, tulikopa lini, kwanini?
Tunaambiwa hesabu za jumla jumla tu, "Serikali imetumia Tri 280 Kulipa madeni". Tumemlipa nani?
Wanajilipa wao, tunaambiwa tumelipa madeni.