Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Mbali ya kwamba ni tabia ya wana CCM kuwatukuza viongozi wa chama chao au wale wanaoongoza Serikali kutokea kwenye chama hicho, lakini imekuwa ni kawaida ya Marais ama wasaidizi/wapambe wao toka chama hicho, kuongea maneno kuashiria kwamba Rais aliyetangulia amemuachia mzigo mzito wa kurekebisha utendaji kazi serikalini Rais alilyepo madarakani.
Ally Hassan Mwinyi alipoingia kwenye madaraka ya Urais, aliingia na kauli mbiu ya "Fagio la chuma" na mpaka wazee wa Dar es salaam walimkabidhi mfano wa fagio hilo. Mwinyi pia alikuwa maarufu kwa kauli mbiu yake ya "Ruksa".
Kwa ivo kwa kauli hii ya "Ruksa" na kitendo chake cha kukabidhiwa fagio la chuma, Mwinyi aliashiria kuwa inawezekana Rais aliyemtangulia, Julius Kambarage Nyerere, alibana sana watu na yeye alikuja kutoa ruksa kwa watu hao. Lakini pia mambo ya fagio la chuma ni kiashiria kwamba Nyerere aliacha uchafu mwingi mgumu ambao kuufagia lilihitajika fagio la chuma.
Alipoingia madarakani Benjamin William Mkapa akaja na kauli mbiu ya "uwazi na Ukweli". Kirahisi tu ni kama kuashiria kwamba aliyemtangulia aliendesha mambo yake bila ya uwazi wala ukweli.
Jakaya Mrisho Kikwete akaja naye na kauli mbiu ya "Maisha bora kwa kila mtanzania". Huyu naye inawezekana aliona watangulizi wake walikuwa hawajaleta maisha bora kwa "kila" mtanzania.
John Pombe Magufuli naye akaja na kauli mbiu ya "Hapa kazi tu" kama vile kiashiria kwamba huko tulikotoka watu walikuwa hawafanyi kazi.
Ni kama vile kila Rais aliyepo madarakani huona kwamba aliyemtangulia kamuachia Urais pamoja na tatizo kubwa sana kwenye jamii. Mbona wakiwa madarakani wanasifiwa sana lakini wakitoka madarakani hushutumiwa na wanaowapokea hayo madaraka??
Nyie CCM vipi??