Nawasihi wasome alama za nyakati mapema, kusema ule ukweli, kutakuwa hakuna wakujitetea, kwani ushahidi wote utakuwepo, na wasije wakaona wanakuja kulaumiwa, la hasha, ila watakuwa wanavuna walichopanda. TBC pia nao wachukue tahadhari, wajaribu kuona vyombo kama CNN, Skynews na vingine vinapokuwa ktk shughuri za vyama vya Siasa. Na hili si kwa TBC tu... Mie nilitegemea hata vyombo vingine vya habari, waache ku copy na ku paste habari za kampeni, ila watafute wanataaluma mbalimbali wawe wanajadili hoja za wagombeni na kuzifanyia uchambuzi wa kina, nadhani hapo Siasa itakuwa tamu kwelikweli. Kwa bahati mbaya, karibu vyombo vyetu vyote vya habari hapa nchini, vinakosa ubunifu huo..