Kila siku lazima niuangalie mwezi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Wakuu Mimi ni kijana ambaye nikiwa natembea barabara huwa napenda Sana kuji reconnect na vitu nature mfano huu mwezi.ndio maana nimekuwa na Spirit kubwa ya kushuhudia mabadiliko napenda kuona wana jf wapya.lazima nizingatie mwezi unavozama kwenye mawingu jinsi ulivyotokea.yaani Cha kwanza nikiamka asubuhi baada ya kumwomba Mungu naenda nje kutazama mwezi.huwa inanipa memory nyingi na kunikumbusha ni Jambo gani kubwa hapa ulimwengu tumeagizwa na manani,Ni upendo kwa hiyo inapotokea nimeuona mwezi nagundua kuwa upo pale kutusaidia na kila siku unafanya kazi zake za record.sifundishi mafundisho ya uongo nataka ujue kuwa ili ufanikiwe duniani unapaswa ukubali mwenyeziMungu ana NGUVU kubwa kuliko yote kwa hiyo wewe utumike 24 hrs/7 days kwenye hii miliki aliyowapa wanadamu.yaani ukubali kuwa uko huru lakini huru katika kujenga hii ardhi.Ni njia kubwa ya ku reboot akili yako na kurestart yote unayojifunza.kwa sababu kizazi chetu kinakabiliwa na tishio la watu kupungua akili.tujitahidi tufanye mazoezi na tule vizuri hio ndio njia namba Moja ya kuzuia kupungua akili.kila nyakati kiwango chako cha ibada kiongezeka.kwa hiyo Mimi nikiuona mwezi hapohapo nakuwa na akili na fikra kubwa kuhusu uzazi,kuhusu maisha.
Kwa mfano binafsi kama Mimi nilikuwa napenda kuona jamiiforum ikibadilika tena na kuwa Kama zamani ambapo tuliona nyuzi zenye madini ya kutosha.baadae kukapoa Sana inaonekana sisi na kina ZERO IQ ndo tunaharibu jukwaa kwa stories nyingi za low thinking capacitors.tukikaa kimya bado nondo hazishushwi.
Ukienda kule kwenye siasa ndio Kuna Fujo balaa unaona Bora hata siasa uende ukabishanie mtaani penyewe hakuna kelele Kama humu ndani.kuheshimiana hakupo kabisa ukija kihivi unachezea za uso.mwisho mtu unakosa kabisa hata nafasi ya kuaminika hata Kama una ma idea ambayo ukiwapa watu wapite wanatoboa.kwa hiyo ninaongea mengi lakini naomba Wana jf tubadilike Mimi ndio kwa Sasa navaa jukumu hili la Nia ya kubadilisha michango,kuboresha Zaid,kupeana michongo mbalimbali watu wengine humu tuna uwezo Sana yaani sisi kazi yote tunaweza tukafanya kwa sababu tuna nguvu Sana ya akili.hata mtaani ukiona kijana yupo jf jua anajielewa Sana tayari ana maarifa Sana muamini mpe kazi yoyote umsaidie atoke kimaisha.akiwa mwaminifu Ni faida kwenu.kimsingi tukae kijanja isifikie Hadi hatua watu wenye maarifa wakaanza kuona uvivu kuandika kwa sababu tu wana jf sio wavumilivu tuwe wavumilivu Kama mwezi tufanye kazi hii Kutoka moyoni itaendelea kutupa faraja.tuvumuliane Mambo mengi muda mchache ndipo unagundua kila kunapokucha siku ya kufa inakaribia.nimemaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…