Kila Siku ukiona unakosa pesa jua Kuna Kitu Kimoja Hakipo Sawa

Silivian

Member
Joined
Nov 13, 2022
Posts
64
Reaction score
103
Wosia wa BABU Mwenye Miaka 103 Kwa Mjukuu Wake Kuhusu Pesa...(Ambao utakunufaisha Pia)...

Ilikuwa ni Mwaka 1999...

Nikiwa Bado kijana Mdogo Mno...

Nilienda kumtembelea Babu yangu Mzaa mama huko Kiomboi-Singida

Lakini...

Bado Nilikuwa na Akili ya Kutosha ya Kung'amua mambo Mbali mbali...

Babu yangu Kila Siku alikuwa akinifundisha Vitu Vingi sana Kuhusu Pesa ila...

Maneno Ambayo yalikuwa hayakauki mdomoni Mwake na bado nayakumbuka Mpaka Leo ni haya Hapa Chini...

"Mujukulu Wane...Zepia Injelio yako ya Mpia"

Haya ni Maneno ya Lugha ya Kinyiramba yenye Maana Hii Hapa...

"Mjukuu Wangu...Tengeneza Chem-Chem yako ya Pesa"

Chem-Chem?...

Ndio...chem-chem ni vile visima vidogo Ambavyo havikauki Maji...

(Sema Hapa wale wa Ushuani sidhani kama wataelewa[emoji3])

Anyway...alikuwaga ananiambia Maneno hayo Mara Kwa mara...

Babu yangu alikuwa anajua Vitu Vingi mno Kuhusu Pesa...

Kwani alikufa akiwa na Miaka 103...na alikuwa Miongoni mwa wazee Matajiri Mno Hapo kijijini

Alikuwa anamiliki Sehemu ya Ardhi Nusu ya Kile Kijiji...

Achilia Mbali Mifugo...(Ng'ombe & Mbuzi)

Boma lake Tu lilikuwa na Ukubwa wa Zaidi ya Heka 5....

NA...

Aliniambia Wazazi wake walikufa yeye akiwa bado kijana wa Miaka 7 Tu...na hakuachiwa urithi Wowote...

....Na Mali Zake Zote alizitafuta yeye Mwenyewe Kwa damu na jasho...

Kuna Baadhi ya Vitu alivyokuwa akiniambia Kipindi Kile nimekuja kuvikuta vimeandikwa Kwenye Kitabu Cha...

"The Richest Man in Babylon"

Siku Moja alinipeleka nje Kabisa ya Kijiji tukaenda Kuoga Kwenye Mto Fulani Huwa una Maji masafi yanayotiririka...

Wakati tunaoga babu akanishika Begani Akanikazia Macho Kisha akaniambia Vitu Hivi...

"Shamanonga (Jina Langu la nyumbani)...Usiache Kutafuta MAARIFA...Ukiona Hupendi Kujisomea Basi jua roho ya Kimasikini inakutafuna"

Akaendelea Kuniambia...

Unakumbuka nilivyokwambia utengeneze Chem-Chem yako ya Pesa?...

Nikatikisa Kichwa Juu Chini kama Ishara ya Kukubali...

Akasema...nilikuwa namaanisha....

"Tengeneza Kitu Kinachokuingizia Pesa Kila Siku Haijalishi ni Ndogo kiasi Gani...Cha Msingi ni Pesa inaingia Mfukoni Mwako Bila Kukauka kama Chem-Chem"

...Nayeye alikuwaga na Biashara zake Ndogo Ndogo Nyingi... Ikiwemo Zile za Kuuza tumbaku zilizokaushwa pamoja na Kutoa mikopo ya Pesa Kwa wanakijiji...

Akaendelea Kuniambia...

Na kipengele Kigumu Zaidi Kuhusu Pesa sio Kutengeneza Pesa kama Jinsi unavyoambiwa...

Ugumu wa Pesa Upo Katika Hivi Vitu Vitatu...

1). Kutumia Pesa...(Spending Money)

2). Kuweka Akiba...(Saving Money)

3). Kukuza/Kuongeza Pesa....(Growing Money)

Akasema...

Kila Siku ukiona unakosa pesa jua Kuna Kitu Kimoja Hakipo Sawa Kati ya hivyo Vitatu Hapo Juu...

I hope umepata Kitu Kipya......
 
Mzee alikupa elimu ya maisha ambayo vijana wa sasa tunaikosa, Tumetawaliwa na aibu, dharau na woga kiasi kwamba hatuwezi kujipambania.
 
1. Earn Money
2. Save Money
3. Invest Money
4.Spend less.

Kanuni ya mafanikio kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…