Watanzania tubadilike! Ukikopa hebu lipa mkopo wako. Umekopa mkopo na unajidai kwamba hautalipa halafu unashinda kanisani au msikitini, sasa sijui unafuata nini huko.
Ingekua zile app za mikopo haziombi address book ya muombaji, ningewasumbua sana. Sasa nasikia wanaomba access ya address book yako, ukichelewa kulipa wanatuma meseji kwa watu wako wote na wanaunda hadi group la WhatsApp wanawaingiza watu wako wote kisha wanaanza kukuchafua.
Itakua aibu kubwa sana watu wangu kujulishwa kwamba nimekopa laki 2 mkopo app halafu nimeshindwa kulipa. Aibu ya mwaka.