Kila ukikutana na mtu ukiwa naye, sifa kibao....!

Kipenzi Chao

Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
99
Reaction score
4
Hivi kwa mfano una GF/BF wako ambaye mlikutana baada ya kumaliza chuo/shule, lakini ikatokea kuwa kila ukikutana na mtu ukiwa naye, ambaye aliwahi kumfahamu, labda huko sekondari au chuoni, na akafahamu kuwa ninyi ni kama nafsi moja, wengi wanakuwa wakimwagia sifa nyingi sana kama vile; mpole, katulia, busara nk, pia na kukupongeza kuweza kuchaguliwa naye kama BF/GF wake....! Je, utajiuliza nini? Utachezwa na machale gani?
 


cjui maana mengine magumu kujibu ati.......................................... hee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Sasa Ndugu yangu ulitaka wakwambie kuwa huyu mwizi, jambazi, kiwembe, mbumbumbu au kilaza wakati anastahiki sifa hizo za upole, kutuli na busara? Hata hivyo huyo anayemsifia ni wa jinsia moja au tofauti? Kama ni jinsia moja kwa nini uwe na wasiwasi? Kama ni jinsia tofauti tafuta mmoja wende naye chemba akuhakikishie asemayo. Hata hivyo haiwezekani kila unayekutana naye ammwagie misifa ya bure huenda kuna ukweli ndani yake.
 
wapo wa jinsi yake na ya tofauti; yaani jinsia zote, lakini inatokea kuwa unakutana na jinsia tofauti naye wengi kuliko jinsia yake...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…