Kila wiki ni taarifa mpya ya kukata umeme kwa kisingizio cha matengenezo! Hivi kweli matengenezo gani yanafanyika kila wiki bila mwisho?
Wateja wenu wamechoka na wamekerwa. Biashara zinaathirika, shughuli za wananchi zinasimama, vifaa vinapata changamoto, lakini TANESCO mnaendelea kutoa taarifa zilezile kila wiki.
Mnatengeneza nini kila wiki?
Tatizo ni nini hasa?
Na ni lini wananchi watapata umeme wa uhakika?
Hatuwezi kuendelea kuambiwa kila wiki kuwa umeme unakatwa kwa ajili ya matengenezo bila kuona suluhisho la kudumu.
TANESCO Mwanza, wananchi wanahitaji majibu ya wazi na huduma yenye uhakika — si taarifa za kukatika kwa umeme kila wiki!
IMEZIDI SASA! ⚡