Kila Wilaya Nchini iwe na timu yake

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Nadhani ni ushauri tu,ili tuinuke ki soka kuna umuhimu wa kila Wilaya nchini kuweka mikakati ya maksudi kuliendeleza soka letu nasi angalau tupande viwango vya Fifa siku zijazo

Kwa kuanza Wilaya ya kinondoni wameshaonyesha mfano,wana timu yao ambàyo inacheza ligi kuu ya Nbc...sasa basi Wilaya zingine zote ziige mfano huo ikiwa pamoja na kutengeneza timu mbili ya wanaume na wanawake waweke na shule pia ya soka "academy"..

Hili litainua hamasa kwa vijana wengi kujitoa katika mchezo huu na ikibidi michezo mingine,haya wameyafanya mataifa ya ulaya na kufanikiwa sana.

Na kwa baadae hizo timu za Wilaya zinakuja toa combine nzuri na kupata timu ya mkoa..ifikapo mapumziko ya ligi kuu kufanyike michuano ya timu za mikoa ili kumpata bingwa wa nchi.

Kwa kufanya hivi nina imani kubwa mbali ya kuibua vipaji kiwango chetu cha soka kimataifa kitakua.

Nawasilisha.

0716399767.
 
mi bado sijakupata unataka kuelezea nini haswa. kwa sababu kama ni timu karibia kila wilaya kuna timu nyingi tu, kila kata kuna timu nyigi pia na hata ngazi ya vijiji vyote karibia tanzania nzima kuna timu za mpira. (japo sijajua mwenzetu unatoka mikoa ipi) tatizo letu Sisi ni mifumo mibovu, taratibu mbovu zinazotokana na wanasiasa pamoja na miundombinu mibovu ya kuchezea mpira.
 
Mkuu miundombinu hamna bado nchi inakopa kuendeleza miradi, kumbuka kwanza wananchi wahasira

Au wewe unaishi Serengeti hujui chochote kuhusu bei
 

Mawazo mazuri, ila usimba na uyanga unadidimiza soka letu kamanda, siku zinakutana simba na mbeya city, mtu wa mbeya atashabikia simba na kuachana na timu yake ya mkoa/wilaya.....japo sio wote
 
Yaani ziwepo timu proper zitakazopata support kamili ya manispaa ili zisimame na kusonga mbele
Hizo unazosema wewe ni ndondo ndio maana hazifiki mbali kwani hazina support ya nguvu.
 
Okay
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…