Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,206
- 18,549
Pimbi tuu
Kabla ya Vipigo ' mfululizo ' vya 5 kwa 4 na Nigeria kisha 2 kwa 0 na Uganda na 4 kwa 2 na Angola Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania ' Serengeti Boys ' aitwae Oscar Mirambo alikuwa kila akihojiwa na Waandishi wa Habari hasa wa Kitanzania alikuwa akiongea Kiingereza ' Kingi ' sana kama siyo mno ila nimeshangaa tokea Timu ifanye vibaya sasa akihojiwa tu na hao hao Waandishi wa Habari ' anakigonga ' Kiswahili mwanzo mwisho.
Je ni nini kimemtokea hadi sasa hivi ameamua ' Kuachana ' kabisa na hiyo Lugha ya Malkia wa Uingereza ambayo alikuwa akiiongea kwa ' Mikogo ' yake yote huku akionyesha kuwa kama kuna Mtanzania anayejua vyema hiyo Lugha vyema kabisa basi atakuwa ni Yeye tu?
Nawasilisha.