Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Kabla ya ndoa, wanandoa huwa na ndoto tamutamu ambazo sio halisi kuhusu ndoa. Kwa kuwa tuna hizi ndoto tamu, tunapokuja kuingia kwenye ndoa na kugundua kwamba tulichofikiria hakipo, ndipo tunapoanza kuvunjika moyo na kujiuliza kama ndoa ina maana.
Kwa kawaida tunachotarajia kukipata kabla ya ndoa, tunapoingia kwenye ndoa hatukipati na hili huvuruga kila kitu. Inaonekana kama matarajio ya wanaume siyo makubwa sana kama yale ya wanawake kabla ya ndoa.
Huenda hili huchangia katika kuwafanya wanaume wasishangazwe sana na kile wanachopambana nacho baada ya ndoa.Inawezekana pia ni kwa sababu wanaume wameshika ‘mpini' kwenye masuala mengi ya kiuhusiano wakati wanawake wameshika kwenye makali.
Hata hivyo badala ya wanandoa kukwaruzana kutokana na kukutana na hali ambayo hawakuwa wanaiota kabla ya ndoa, inabidi wajifunze maana ya ndoa wakiwa ndani ya ndoa yenyewe. Inabidi wakubaliane na yale ambayo hawakuwa wameyatarajia na kujifunza kupitia kwayo.
Badala ya kukimbia hali halisi ya ndoa, ni vyema kujifunza na kuikubali, ni vyema kubadilika ili kwenda nayo na sio kutegemea hali hiyo ibadilike.