Nakubaliana na wewe lakini hata wao huwa wanakunywa. Kuna tatizo zaidi ya hilo. Tukiondoa ukiritimba wanaweza kufanya vizuri zaidi.
Mfano: niliongea na wachezaji toka CCP moshi, wengi wao ni wanariadha wazuri sana lakini hawapati muda wa kufanya mazoezi. Utakuta mtu aling'ara kwenye mashindano fulani halafu viongozi wa jeshi wanawachukua kuwapa ajira. Wakishaajiriwa tu sheria za jeshi palepale. Unapelekwa lindoni wakati wa ratiba ya michezo. Unategema huyu mtu atakuwaje. Anaweza kweli kwenda lindoni na wakati huo huo kufanya zoezi? Hata ruksa za kushiriki mashindano ya kimataifa huwa ni shida kwao!