Kilichofanya TSH istabilize Against USD

Mambo makubwa matatu yaliyochangia shilingi ya Tanzania kupanda thamani ikilinganishwa na dollar ya Marekani ni benki kuu kuingilia soko na:
1. Kupandisha "Base lending Rate"- Nadhani kwa 100 basis points
2. Kupunguza "Forex Net Open Position" kwa mabenki kutoka 20% mpaka 10%
3. Kuongeza "Statutory Minimum Reserve" kwenye deposits za serikali kutoka 15% to 30%.

Hizi measures zote kwa ujumla zikiwa na lengo la kupunguza fedha nyingi zilizo kwenye mzunguko kwa ajili ya ku-control "inflation" na kupungua kwa shilingi katika mzunguko kumesababisha watu wauze sana dola walizonazo ili kupata shilingi.

Jambo lingine ni kwa serikali kupitia benki kuu kuwauzia dola moja kwa moja waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia benki zao .
 
Uwezo wa kuifanya dola inunuliwe ata kwa tsh 100 tunao ila kuna watu wanafaidika na ughali wa dola.
Iweje mauzo yetu ya dhahabu yanafika $ 2.2 billion na bado tunahangaika kustabilize ela yetu.
Tatizo tuna wataalamu wengi wa political economy and not really economists!
 
Jambo lingine ni kwa serikali kupitia benki kuu kuwauzia dola moja kwa moja waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia benki zao .

makampuni ya mafuta kununua dola BOT bado ni optional

kwa wafanayakazi wa makampuni hayo wanaotaka % kwenye uagizaji bado wanaenda direct commercial banks ambako kuna BOT compliance zisizokuwa mandatory sana na zaweza kuchezewa linapokuja suala la exchange rate
 
 
Da. Sisi tunaolipwa mshahara kwa dolllar hii habari si njema kabisa. Huyo atakuwa dr mwamba kaja na mikakati hiyo. Ee mola haribu mipango hiyo ili shillingi iendelee kuporomoka T
 
Da. Sisi tunaolipwa mshahara kwa dolllar hii habari si njema kabisa. Huyo atakuwa dr mwamba kaja na mikakati hiyo. Ee mola haribu mipango hiyo ili shillingi iendelee kuporomoka T
Si bure
 


Nina mashaka sana na maana halisi ya maneno katika red hapo juu. Commercial banks nyingi ni private sector operations. Hilo linaweza kuwa lilikuwa shimo la capital flight, na hao wezi watakuwa wamezitafuna kwelikweli hela za nchi yetu. Kwa kweli tunahitaji Paranoics wawili watatu katika mfumo wetu wa management ya uchumi. Tumekaa muda mrefu mno bila kuliona hili. Unaweza ukute pengine rate ya dola inatakiwa hata kuwa 800/-. Tuishukuru BoT, hata hivyo kwa kufukia shimo hilo, japo ni kwa kuchelewa sana, kama hii taarifa ina ukweli.
 



Thanks for this more scientific explanation. Kwa nini tulichelewa kufanya hili?
 
Shilingi inaweza kuimarika zaidi na zaidi ikiwa BoT itakuwa na utashi wa kukatisha maslahi ya wakubwa. Ikiwa BoT itafanikiwa, pamoja na mambo mengine, kuzuia matumizi holela ya Dola (kwa sasa kuna taasisi za elimu; maduka n.k yanayotoza malipo kwa Dola). Dola haotoweza kushuka thamani ikiwa uhitaji wake ni mkubwa.
 
Matumizi makubwa ya dola kwaajili ya msafara wa rais na kundi kubwa la kumsindikiza muheshimiwa.
Pia exportation of primary raw materials.
 
JUST mnahitaji ujazo wa dola uwe mwingi kwenye soko, kwa kuzalisha zaidi ili mpate forex . Mngeweza kuingia mikataba nizuri ya ubinafusishaji mngeweza kuwa mnzalisha bidhaa nyingi na kuuza, mngeweza kuuza dhahabu na kupata proceed kupitia local banks ambapo mngekua na billions of dollars rtaer kuwa na vijisenti vinavyorudi kulipia matumizi, kilimo mngeimarisha ili kuuza kahawa na nk. Pia kutegemea sana misaada pia ni shida wapunguzapo misaada ina maana kadola hakaji. Even though uchumi wa dunia ni tete, ulaya wanalia lakini kwa ali ya kawaida ilikuwa ndio kipindi cha nchi zenye rasilimali kupaa kiuchumi. Chimbeni dhahabu mbadilishaje na wese, tumieni gesi msinunue mafuta, tumieni makaa ya mawe msinunue mafuta. Waambieni wawekezaji kuwa 50% ya proceeed ya revenue kutoka mali asili ilipwe kupitia benki zilizopo Tz mtaona mabadiliko na pia acheni kutuma pesa nje wekezeni humuhumu.
 
ila kwa sasa mlio hifadhi dola nadhani ni furaha kwenu kwa shilingi ya tz kushuka thamani

kwani kwa mtaani (siyo bank) sasa hivi inabadilishwa kwa bei gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…