TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,345
- 6,970
Kumekuwa na mitazamo ambayo inaambatana na lawama kutoka kwa watu tofauti tofauti wakiendelea kuwalaumu ndugu zao au wazazi wao eti kwanini wamekuja mjini hasa Dar es Salaam miaka ya nyuma ambayo kila kitu kilikuwa cheap (rahisi) na hawana maeneo, nyumba Wala ukwasi ambao wanadai Kwa miaka hiyo ilikuwa rahisi kupata!
Unakuta huyo mtu anayelaumu, amekuja Dar es Salaam huu ni mwaka wa 20 na zaidi hana chochote cha maana!
Ok yeye alishindwa kuwa tajiri, wewe kimekushinda nini kuwa tajiri leo, kilichokushinda kununua uwanja na maeneo makubwa hadi sasa ni nini?
Vijana acheni lawama, mambo si rahisi kama mnavyodhani! Tena mbaya zaidi unakuta ukoo wenu au familia yenu haina mkondo huo wa pesa ndiyo utapata taabu sana!
Familia nyingi zilizoendelea miaka hiyo na zinazoendelea miaka hii, ni lazima walikuwa na ka-uwezo tangu mwanzo hivyo walishikana na wanaendelea kushikana mikono!
Ni ngumu mno mtu hakuwa na kitu kabisa akaanza moja hadi kuwa tajiri,kama ambavyo imekuwa ngumu kwako!,vinginevyo uenda ukawe Tapeli au Mwizi!