Tea Party
JF-Expert Member
- Oct 5, 2019
- 658
- 1,133
Mimi ni mmoja wa makada wa CHADEMA ambao tulikuwa tunasimamia uchaguzi mkoani Geita eneo la NMC
Kama moja ya wasimamizi wa uchaguzi huo, mara baada ya majina kubandikwa nimegundua udanganyifu mkubwa uliofanywa ikiwemo uwepo wa wapiga kura hewa takriban 300.
Orodha ya wapiga kura walioandikishwa ambao walikuwa ni 647 ilikuwa hairandani na majina yaliyobandikwa ambayo ilikuwa ni. 947.
Binafsi nimeenda kwenye kata ya Kasamwa na Kanyala kulalamikia watendaji wa kata kuhusu mchakato ulivyofanyika kiwizi wizi lakini hakuna majibu yanayoeleweka.
Soma pia: Baadhi ya Halmashauri za mkoa wa Geita zinawaibia watumishi posho zao kwenye uchaguzi, TAMISEMI fuatilieni
Ninachoambiwa ni kuwa inabidi nipeleke mapingamizi. Sasa najiuliza kama walijua kuna masualaya kuweka mapingamizi, kwanini walikuwa wanatuweka mawakala?
Wizi na udanganyifu uliofanyika ni dharau na matumizi mabovu ya kodi zetu ambazo sisi wananchi tunaipa serikali.
Tunaiomba TAMISEMI ifuatilie na kuwaajibisha wote waliohusika na wizi huu kuanzia Mkurugenzi ambaye anasimamia mpaka watendaji wa kata.