Tatizo lenu kwa wale msio na experience ya kutafuta kazi ni moja tu! nalo ni KUSIKILIZIA!!!! mnapenda sana kusikilizia application na interview mnazozifanya!!! Wenzenu tulio na uzoefu wa kutafuta kazi bila kupata kwa miaka kadhaa sasa huwa hatusikilizii!!! Tunadondosha CV/application mahali halafu tunapotezea kama hakuna tulichofanya!! Inafikia wakati unaitwa mahali Interview, halafu unajiuliza "ni nani alipeleka application yangu kule!!!" coz', baada ya kudondosha application, ukapotezea hadi unasahau kabisa kwamba ulipeleka application!! Hata baada ya interview, wakongwe huwa tunapotezea kwamba kuna mahali umefanya interview! ukipenda kusikiliia haya mambo, mtaugua ugonjwa wa moyo brodaz!! Sana sana, unaweza kusikilizia maximum mwezi mmoja...sasa wana mnasikilizia hata kazi mlizoomba tangu June?!