KILICHOJIFICHA HIFADHI YA NGORONGORO
Katika hali isiyokuwa ya kawaida hivi karibuni kumeibuka mijadala mbalimbali kwa wale wanaojiita wanaharakati (Uchwara) wa kutetea haki za watu wa Jamii ya kimasai waishio Ngorongoro.
Hapa kuna hoja kubwa inayozungumzwa na wanaharakati hao kuwa wanaotaka Wamasai wahamishwe kuwa wanakosea lakini wanaharakati hao wanakubali kuwa Jamii hiyo inakumbwa na changamoto nyingi. Mfano kila uchwao watoto na watu wazima wanakufa kwa kushambuliwa na wanyama wakali kama simba na chui.
Pia wanaotaka Wamasai wasihamishwe ndio wanaofaidika na huduma zinazopatikana pale Ngorongoro kwa wenyeji maana Ng'ombe wengi wanaofungwa katika maeneo ya Ngorongoro sio mali ya Wamasai bali Wamasai wamegeuzwa manamba na Matajili wa Arusha na Wanasiasa sababu ndio sehemu pekee malisho ya mifugo ni bure hivyo Matajili hao wanatumia kama fursa ya Wamasai kuendelea kubaki katika maeneo hayo.
Tafiti iliyofanywa na NBS Mwaka 2017 inaonesha ni asilimia 3 tu ya wenyeji ndio wanamiliki mifugo pale Ngorongoro.
Pia Jamii ya Masai wamegeuka kuwa ombaomba katika maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro sio tena kivutio cha wageni bali wamekuwa kero kwa wageni wanaopita katika Hifadhi hiyo
Lakini kubwa na baya zaidi WATALII wanaopita Ngorongoro kuelekea Hifadhi zingine wanatakiwa kulipa dolla takribani 70 kama kiingilio cha kukatisha mbugani lakini cha ajabu wakiwa njiani wanajionea kundi kubwa la Ng'ombe, Mbuzi na kondoo badala ya Simba, chui na Tembo ni Jambo la kusikitisha sana
Ushauri nyie wapiga kelele maarufu kama wanaharakati Mchwara Mjitahidi kwenda kujionea Hali ilivyo kwa ndugu zetu Wamasai.
#OkoaMasaiNgorongoro