Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa


Brah Maggid skiza mkuu,mimi sina chama. Na unaposema "Tuwaachie wengine wasome na waamue" una maana nimewazuia "Hao wengine" kufanya hivyo? Kuna mtu nimemwambia kuwa asisome na kujiamulia humu ndani?Hao wanaotofautiana na mimi hata kama tuko chama kimoja kipi hicho? Na kama umeshasema umepigiwa simu na hao chadema kukushukuru,then ulitakiwa ufahamu kuwa utofauti huo unaonyesha wazi kutokuwa kwangu chadema ama kutokuwa mshabiki tu na mfuata upepo ka bendera. Mwenyekiti wenu anaposema asilimia 70 ni wafuata upepo na wewe unataka kuja kujiaminisha kwamba huo ni ukweli? Once again ujue kuwa si wote wenye vyama humu ndani,na kwa hivyo si wote wenye kupenda bias...Na huo ndo uzur wa JF mkuu. Sijaelewa haswa ni kipi ulichokubaliana na kipi ambacho hukubaliani na sababu za either or sijaziona,otherwise hakuna mantiki unapodai "Tukubaliane kutokubalina" na wakati hujaeleza makubaliano hayo ya kutokubaliana ni yepi!

Nitashukuru kama utarudi kwenye hoja ya msingi ili kuepeusha upotevu wa muda ambao kusema kweli ni adimu kwe wengi wetu,keep in mind kuwa hata mimi siyo kwamba sikubaliani na yote uliyoandika...La hasha....Ambacho sikubalini nacho ni hizo analysis za hayo madhaifu,kwangu mimi nimeona kama ni strengths ama nguvu zake/zao rather than weaknesses...Hao wanachadema waliokushukuru ni kwa uwezo wao wa kufikiri,na hivyo si lazima na mimi nifikiri kama wao....Si wote ni mashabiki wa group think humu JF na si wote ni wanachama wa vyama vya siasa.
 
Maggid

Kwa jinsi ninavyokusoma, unaonekana kutafuta zaidi MASLAHI BINAFSI kuliko kuhamasisha MASLAHI YA TAIFA kwanza.

Ni kipi kibaya anachoongea Slaa, kiasi kwamba umwone kuwa haifai kuwa kiongozi? Ni mangapi aliyaahidi JK, lakini hakutekeleza? Alitoa onyo kali kwa mafisadi, Desemba 30, 2005, kwamba, yeyote atakayetumia nafasi yake ya madaraka kwa maslahi binafsi, ANGEWAJIBISHWA! Wangapi wamewajibishwa?

Tuna machungu kaka, nchi yetu imeuzwa jumla. Madini wanavuna wageni; tunaambulia vijisenti. Mafuta, wanakuja kuvuna wageni, hatutaambulia chochote... hata Nigeria wana mafuta, lakini SI YAO! Hiyo gesi...

Nchi tajiri, watu wake maskini!

HUONI HAYA kutetea maovu? Nilidhani, na Uislam wako, UNGEUPINGA UFISADI, lakini wewe wasema Waache Wachukue Chao Mapema?

Unasikitisha!

-> Mwana wa Haki
 

Ndio tatizo lenu 'expert analysts' wetu wa Kibongo:UJIKO,SIFA,etc.Kwako la muhimu zaidi ni hizo "simu za sifa kutoka watu wa Chadema" kuliko constructive criticism ya wapi makala zako zinakwenda harijojo na kwanini wengi wa WANA-JF wanakuona huna tofauti na viumbe kama Makamba au Tambwe hizo,only that they are officially known as mouthpieces for mafisadi and you are not!

Let's be realistic.Umejuaje kuwa hao waliokupigia na kukupongeza "ni watu wa Chadema"? Je walijitambulisha kama watu wa Chadema au unawafahamu kuwa ni watu wa chama hicho?Maana inawezekana kabisa waliokupigia ni watu wa Habari Leo kama sio Daily News au pengine ni JK mwenyewe,mama Salma,Ridhiwani,Kinana,Tambwe Hiza,Issa Michuzi,Makamba,Brigedia Jenerali Shimbo,John Tendwa na "wengineo" kisha wakajitambulisha kuwa "watu wa Chadema".Honestly,I doubt kama ulipigiwa simu at all,sio kwamba sikumini bali I wouldn't trust Mhariri wa Uhuru/Mzalendo "anaposifiwa kuhusu Chadema".It simply smells fishy.

Na hujatufafanulia kama sifa hizo zilihusu nini specifically.Je ni jinsi "ulivyoweza" kuonyesha "udhaifu wa Dkt Slaa" au...?Na kati ya hao "wana-Chadema waliokupigia simu" hakuna aliyekuomba umtendee haki Dkt Slaa kwa kutoa similar analysis kwa Kikwete ie "sifa" na mapungufu ya Kikwete?

Can you try to do that,please?Maana kama ni rahisi kuchambua sifa na mapungufu ya Dkt Slaa ambaye ni mara ya kwanza kwa yeye kugombea urais basi lazima itakuwa rahisi kwako "self-proclaimed expert analyst" kutupa uchambuzi kuhusu incumbent President Jakaya Kikwete ambaye amekuwa madarakani kwa miaka mitano sasa.Nakumbuka ile assessment yako ya miaka mitatu ya JK madarakani lakini kqa faida ya jamii ni vema "tujifanye hatukuiona" ili tuweze kukutendea haki katika assessment yako ya sasa kuhusu Kikwete.

Pleeeez!
 
Kwanza nimshukuru Maggid kwa kuanza kuona ukweli kwa mbali hususani baada ya kusoma makala yake moja ambayo ilitumiwa takwimu feki za mwaka arobaini na saba katka kujaribu kubashiri ushindi wa Tsunami kwa JK.


Hivyo kura kwa Chadema inahitaji iwe ya
three piece suit
ili mageuzi ya katiba na mengine kuweza kutekelezeka bila zengwe hata kidogo.

Ukweli kama JK ana nia ya kuacha urithi wa kukumbukwa asicheze hata kidogo na matakwa ya watanzania kwa kutumia jeshi na watumishi serikalini. Vinginevyo ICC itamdaka na hatungependa tufike huko.

Akabidhe Nchi yetu kwa amani na aonyeshe ukomavu wa kisiasa kwa hilooooooooooooooooooooooooooooooooo

That is his only chance to leave a memorable legacy huko nyuma madudu yake tutayasahau kwani

Africans are by nature very forgiving................
 
Makala imetulia ingawa ina mapungufu mengi kama wachangiaji wengi walivyoeleza.
 
Wengi wetu tukielezwa ukweli hatutaki kuubali. Kushinda km wengi wanavyotaka kujiaminisha si suala la rahisi. CHADEMA hawakuwa na mikakati ya kutosha kujiandaa na kushinda. Mgombea wao ni bora na anaweza kusimama Jukwaani akapambana lkn mgombea huyu amekurupuliwa ili agombee kwahiyo hakuwa na maandalizi ya kutosha. Ukisikiliza Kampeni nyingi za CHADEMA maneno yamekuwa yakijirudiarudia. Niliwahi kulisema hili mwanzoni kuwa CHADEMA wapo too general. Hawaonekani kuyafaham matatizo ya wananchi kiundani. Yaani hawawezi kuainisha vipaumbele vya kila eneo la nchi hii wao wanamtazamo ambao ni general. Yapo maeneo ukitaja suala la umeme au barabara watakuelewa zaidi kuliko maeneo mengine.
Ukiachana na hili, wengi wameonekana kupondea analysis ya Maggid tena wengine bila hata ya kusema kwanini. Mfano Maggid anaongea kwamba CHADEMA ni ngome ya CCM; huu ni ukweli kwa sababu CCM tayari mkoani Iringa inamajimbo 3 imeshayakamata kabla ya uchaguzi na CHADEMA wanaonekana wananguvu kwenye majimbo 2 au 3. Yaliyobaki km Kalenga, Kilolo nk. kule CCM wamechukua. Kwahiyo hata km CHADEMA watapata majimbo hayo 2 au 3 bado Iringa itaendelea kuwa ngome ya CCM.
Kuhusu uongeaji wa Dr Slaa, hapo natofautiana kidogo na Maggid. Kimsingi Dr Slaa anaangalia hadhara iliyomzunguka. Maana ukiongea bila kutukana kuna baadhi ya watu wanaona hujafanya kampeni bado.
 
 
Hii ndio huwa naita crap... ugoro ... upupu... pumba. Chadema hawayafahamu matatizo ya wananchi??? Unaota wewe au unaoteshwa? CCM yako unayojikomba nayo inayaelewa? Wewe nishakuambia ni social climber na unachumia tumbo lako.... basi! Hata hilo blog lako la kifisadi litakudodea siku moja!!
 
Kama niliposema huko nyuma, Maggid kama watanzania wengine ana haki ya kuzungumza kitu anachokifikiri au kudhania, lakini lazima naye lazima aheshimu haki ya wengine kupingana na kile anachosema. Wiki mbili zilizopita Kikwete alikuwepo hapo Iringa, tuliona kwenye Blog yake picha mbali mbali zilizomwenyesha yeye mwenyewe kwenye huo mkutano; lakini, cha kushangaza hakutoa analysis yeyote kuhusu strength na weakness za Bwana Mkubwa. Zaidi ya hayo, siku tano zilizopita Mtoto wa Kikwete alifukuzwa hapo shuleni Mwembetogwa na vijana waliopinga yeye kufanya mkutano katika eneo la shule na muda wa masomo, Maggid akuthubutu hata kupost picha kwenye blog yake! Mbaya zaidi ya haya yote yametokea katika uwanja wake wa nyumbani (Iringa). Ni vitendo kama hivi vinawapa watu shida kujua dhamira yake haswa katika suala hili zima la uchaguzi. Kama ameshindwa hata kuandika chochote kuhusiana na JK kumpigia kampeni watu kama Chenge , Mramba na Rostam anapata wapi credibility ya kumkosoa Dokta?
 
Kweli wewe macho mdiliko maana umeshindwa hata kuona nani aliyepost. Binafsi sina blog na sijawahi kublog labda bahati kuu nilionayo katika mjadala huu ni kuwa mie ni mwenyeji wa huo mkoa. Kwahiyo naifaham fika Iringa. Nimezungumzia kuyaainisha. Hebu jipe fursa ya kusoma Ilani ya CHADEMA. Imekuwa too general such that they cannot be held accountable. Ukienda Dabaga Iringa utakuta wanahangaika na soko la matunda lakini ukiwa kule Lupembe wao wanazungumzia zaidi chai. Kwahiyo kutoa maneno yanayofanana kwa wananchi wa maeneo haya ni kutowatendea haki.
Lakini pia, pamoja na ukubwa wa mkoa wa Iringa unafaham kuwa mgombea wao wa Urais amefanya mikutano mingapi?
 
Wewe haupo sahihi. Unajua shule ya Mwembetogwa inamilikiwa na CCM? Kwa kukusaidia ni kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Ipogoro na pia si km lilivyoripotiwa na vyombo vya habari.
 

Kwahiyo Dkt Slaa akirudiarudia kutaja sera za Chadema ni mapungufu lakini kwa JK kurudiarudia ahadi alizoahidi mwaka 2005 ni mafanikio!

Hivi kama Chadema ingekuwa mtaji wa CCM kama mnavyotaka kutuaminisha,kwanini basi JK na CCM wanahaha na helikopta zao 3?Kwanini taasisi za utafiti (na sio watafiti feki kama akina Mjengwa) zinashindwa kubainisha nani anaongoza kura za maoni iwapo Chadema ni mtaji wa CCM?

Mwaka huu mmekaliwa kooni.Mtajaribu kila mbinu ikiwa ni pamoja na "kuisifia Chadema japo kiduchu" lakini mkae mkielewa kuwa 2010 HATUDANGANYIKI
 
Kiuhalisia CCM hawana jipya na hilo halina ubishi. Ahadi hizi ni zile zile miaka nenda rudi kama wanavyofanya katika Bunge la bajeti. Lakini strategy za kuwaong'oa nazo bado ni loose. Inahitajika organisation ya kueleweka yenye kuweka wanafiki kando, wabaguzi wa kidini au kikabila pembeni, maslahi ya nchi mbele, ubabaishaji na udikteta mbele na maadili yaliyotukuka hapo ndio nchi yetu itakombolewa kwa sasa ni blah blah yu ndio zinaendelea.
 
Sikutegemea mwandishi wa Makala kama Majjid kuja na mawazo kama haya. Nilifikiri kuwa wewe ni mwanamapinduzi lakini kwa hili nakutoa. Jiulize, Dr Slaa ameongea kwa dk 43, mangapi ameongea, kwa muda huo ataanza kutangaza kiongozi wa shina wa Chadema pale Iringa mjini. Kama wako mia muda huo utatosha.

Pia waliohudhuria waliambiwa na nani kuwa Dr Slaa atafika. Au hujiwi kuwa viongozi wao wa shina ndo walioshiriki kuwajulisha. Kumbuka kuwa viongozi wa upinzani kwa hali ilivyo sasa ni CCM wenyewe. Inawezekana nawe umo kwenye kundi hili ila hutaki kuonekana kwa wapambe wenzio.
 
Mimi nakubaliana na wanaosema kwamba hii analysis ya maggid ni very cheap na low level kwa sababu mbili kubwa, kwanza uamuzi wake wa kutokua scientific kwa kuamua kwamba analysis ni ya Slaa peke yake na pili ni ya analysis yenyewe kuwa opinionated. Na inapotokea hivyo nadhani si hekima kuwa mkali kwa kuwa kunakaribisha analysis za yeye pia kwa namna hiyo hiyo ambazo naona hapa anaziona kama criticisms. Nafikiri alichotusaidia ni kujua kwamba kumekua na kuvunjwa rekodi ya uhudhuriaji, kitu ambacho ni cha msingi kwetu, na kile cha kufuta woga kwa wafanyakazi wa serikali. Mwisho angeendelea tu kumtakia heri na kuwatia moyo wanachadema na watanzania wengine wote katika kufanya maamuzi sahihi ifikapo Octoba 31 2010. Namshangaa hakuzungumzia hotuba na pambo za JK juu ya Rostam Aziz, public enemy number ONE na kufanya analysis ya hotuba hiyo na udhaifu wake na msemaji wake na chama chao, angetusaidia pia kutusisitizia hatari iliyopo kwa sisi na vizazi vyetu cha kumchagua agent wa mafisadi, shujaa wa kuwasifia washenzi nambari one na adui wakubwa wa vizazi vyetu na nchi yetu.
 
Sawa majidi mjengwa kwa upembuzi wako ,na sisi wengine tulikuwepo umeishawishi akili yangu ikate rufaa juu ya mambo kadhaa katika upembuzi wako ulitakiwa kuenda mbali zaidi katika fikra zako hususani hao mabalozi wa nyumba kumi ,mabalozi unaowazungumzia hawako upande wa ccm kwa taarifa , kwanza ujio wa kikwete uliwajeruhi mioyo yao na kutonesha makovu va machungu waliopata wakati wa kura za maoni zilizofanyika agosti mwaka ndani ya chama cha mapinduzi ilikuwapata wagombea ambao wangemenyana na wagombea wa upande wa vyama vya vya siasa vya upande wa upinzani.kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 31 october wa 2010..

kwa taarifa mabalozi wameunda mtandao ambao utaiadhibu ccm katika uchaguzi mkuu mwaka huu,kwanini wanadai kuwa ccm inawatumia kama mihuri kuwapitisjha kwa kishindo lakini hawa neemeki na matunda ya kazi wanayofanya kuwasaidia wagombea kushinda uchaguzi ,wao hawanufaiki na chochote kutokana na nafasi zao za ubalozi ,pia mabalozi hao wamlalamikia kitendo cha jk kuwa kalisha mada mrefu pale katika chuo cha mafunzo ya ufundi veta Iringa aliwaomba akutane no mabalozi ,wenyeviti ,makatibu wa mtawi na wazee mashuhuri mjini Iringa walitakiwa wakutane saa kumi alasili kilichotokea JK alifika saa mbili usiku baadhi ya mabalozi na wenyeviti waliamua kuahirisha na kuondoka kwenda kwao .kama haikutosha mbabalozi hao wliambulia soda moja wawo walitarajia kupewa angala kipoza machungu ,kibauya zaidi hawakurdihiwa gharama za usafiri wakati walipofika hapo veta .chukizo lingine ni pale walipo kaa hadi saa tano usiku na kutelekezwa kwenye vituo vya usafiri blia kuwafikisha nyumbani kwo mifano michache wale wanokaa kigonzile walibwagwa TRM KIHESA usiku huo ,wale wanao kaa igeleke walibwagwa kihesa kilolo na kuanza kuchpa mwendo hadi igeleke umbali wa km 7 hadi huko mdongo kwinama.wengine waliachwea nduli ambao walitakiwa wafikishwe huko nymg;uku ubali wa km 8 haya ni baadhi ya mchungu walinao hadi leo wamepa wamesma nilazima waifundishe adabu ccm.

Kuhusu kumtaja monica mbega kitabu cha maadili kinakataza kumtaja mgombea jina lake kwa taarifa yako,halafu pia kitabu hicho kina mapungufu kwa sababu wawakilishi wa vyama walikwenda kujadili na kupitia mapungufu hayo msajili wa vyama alipoambiwa upungu huo wakuta mtaja jina yeye hakukubalina kwa sababu anajua vyama vya siasa wanajua wahalifu wengi ndni ya chama cha mapinduzi sasa hiyo nikinga kwani hata jk ni mhalifu mkubwa umetuibia sana na washirika wake .

Wana Iringa hawezi kumchagua monica mbega hata umpigie upatu hapati watu wamemchoka anagawa fedha elfu kumi kwa madereva tax pale posta lakini wameapa hawampi kura .

Yawezekana wewqe hujui kusoma watu taarifa anazo toa Dr zinawaingia watu akilini ulitake aseme nini sasa atukane watu ,watu hawakujazana tuu umesahau kuwa makumi kwa maelfu ya watu waliokuwa mwembetogwa walifika pale tangu saa tano asubuhi wameshida wanamsubiri SDr Slaa .hawkuletwa na malori kama wanavyofanya ccm ,wahwakuvutiwa na vikundi vya kisanii kama wanavo alika the comerdy ccm .

Dr Slaa kwa taarifa yako anajua matatizo ya wananchi anajua umaskini umesababishwa na nini ndiyo maana anataka kwenda ikulu sio kaka yako anaulizwa kiini cha umskini katika nchi yako anasema na yeye hajui sasa ameenda kufanya nini Ikulu ameendq kuuza sura .

kweli nimeamini falusafa isemayo maneno ya mtu ndiyo mawazo yake kweli hayo ni mawazo yako .siamini kama Dr Slaa anweza kumtoa nje ya mada msikilizaji ukumbuke kuwa Dr Slaa anaongea na watui wakila rika na elimu kwa hiyo maswala ya epa iptl meremeta deepgreen ni uhimu
 
maggid

huoni haya kutetea maovu? Nilidhani, na uislam wako, ungeupinga ufisadi, lakini wewe wasema waache wachukue chao mapema?

Mwana wa haki

haya hivi unamjuaje mtu kuwa ni muislamu? Umekuwa mnajimu na wewe?
Hapa bila shaka panaoneka pananuka udini ile mbaya!!!!
 

crap!!!!!!
 

Ndugu zangu,
Mimi kitaaluma ni mwalimu. Na Mwalimu anaweza kuwa mwandishi kama mtu mwingine ye yote. Mimi si mwandishi wa habari. Ni mwandishi wa makala magazetini. Ye yote yule anaweza kuwa mwandishi wa makala. Uandishi wa makala hausomewi.

Kwenye ualimu nimejikita kwenye Elimu ya Watu Wazima. Ninapokutana na kufanya kazi na watu wazima approach yangu inafanana na ninachofanya hapa. Nimechokoza mada zinazotusaidia kupata maarifa zaidi, ni sehemu ya kazi yangu. Nitaendelea kuja na mada, si za uchochezi , bali kuchochea mjadala.

Nakumbuka nilipokuwa mdogo pale Ilala,Dar niliwashawishi watoto wenzangu tufanye kitu kisicho cha kawaida. Siku moja tulikwenda kuangalia mechi ya soka Uwanja wa Karume. Katikati ya safari kwenye Mtaa wa Lindi tugeuze njia kwa pamoja na kuanza kurudi tulikotoka. Tukaanza kuwakabili watu wengi waliokuwa wakienda mpirani. Katika muda huo kila mmoja alikuwa akielekea mpirani. Na wengi tuliokutana nao walitushangaa na wengine kutuuliza kama mechi imehahirishwa. Basi, hata tulipogeuza na kuendelea na safari tukawapita watu waliokuwa wakiendelea kujadili kama mechi imeharishwa au la!

Kama mwalimu, furaha yangu ni kuliona darasa liko hai kimajadiliano. Naamini katika ´upumbavu' wangu huu na elimu yangu ndogo bado naweza mara moja moja kusababisha mijadala kama hii. Mijadala inayotuwezesha kupata maarifa zaidi.
 

Nakubaliana kabisa na wewe. Tusiwe kama maji kufuata mkondo kwenye haya maswala ambayo hata kama tukiamua kumpa kura kiongozi fulani, ni muhimu ayafahamu kama ni ya muhimu kuyatumia kuiunda timu itakayoweza kutuletea matamanio tunayiyataka. Fikra zetu hizi zina mchango mkubwa sana kwa hayo na hasa pale inapotokea kuendesha debate ambazo zinafanya mawazo mengi zaidi kujitokeza.
Kikubwa pia tusiishie kujadili tu. Tukapange foleni pia kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…