Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Nonsense.
 
Maggid Endelea na makala zako...Wenye akili huru wataelewa. Kingine hii kusema JF wengi wamekupinga...isikushtue saana. Wengine ni wale wale wanajina zaid ya 10, mengine ya kujifanya wema, na mengine ya kuwatukana watu. kama Mzoefu wa JF, hili haliwezi kukushtua.

Sisi Wengine mtu anapotaja madhaifu yako, unayachukulia kama challenges, ili next time usizirudie...!!!

Mwisho ifikie Mahala tukubaliane kutofautiana, Siku hizi imefikia ukiwa na msimamo tofauti na wengine basi maneno ya ajabu eti kutumiwa na mafisadi ...etc utaandamwa nayo...ila usikate tamaa.
 
haya hivi unamjuaje mtu kuwa ni muislamu? Umekuwa mnajimu na wewe?
Hapa bila shaka panaoneka pananuka udini ile mbaya!!!!
karibu jukwaani, mbona unafanana na malaria sugu!!!!
 
Maggid Umekuwaje?
Watu wanachangia mada yako wewe una-loose temper! Umeanzisha mjadala, jibu hoja kwa hoja hata kama wachangiaji hawa kutumia lugha ya kiungwana-tumia busara kuipa nguvu huja yako siyo jazba. Umelikologa huna budi kulinywa! Wewe ni mwadishi mahili lakini inaonekana umechambua mkutano wa CHADEMA tu na siyo CCM na vyama vingine. Kwanini, tupe maelezo!
 
Na Maggid Mjengwa,



Iringa ni ngome ya CCM.

Duh hii ulioanza nayo ni kali......trust me hii ni historia sasa. tumia neno ilikuwa.

" Ndugu zangu, leo mtoto anakwenda shule anaambiwa abebe na ndoo!" Alisema Dr Slaa.
Niliwasikia wasikilizaji wakimalizia na " mafagio, makwanja…"
Hapo Dr Slaa aliweza kupenya kwenye kero na matatizo ya kila siku ya wapiga kura. Na ni mambo haya ambayo wapiga kura wanayaelewa zaidi kuliko kashfa za EPA, IPTL, Deep Green na nyinginezo ambazo akina Dr Slaa na wanasiasa wengine wameshindwa kuziweka katika lugha nyepesi ikamfanya mpiga kura wa Kihesa awaelewe. Mpiga kura ambaye bado anaumiza kichwa kila siku kutafuta senti za kununulia mafuta ya taa na michango ya madawati ya watoto wake. [/QUOTE]

Loh! kwa hiyo wana-Iringa wako tayari kuipigia kura CCM ili mafagio na makwanja yapatikane lakini EPA, IPTL, Deep Green....hayawahusu hayo wala hawana haja nayo....wacha mafisadi wapore tu sio shida...cha msingi ni mifagio na makwanja....duh!!!

Hapa ndo tunasema kila siku ujinga wa mtanzania ni mtaji kwa CCM.


Kuna wakati kwenye hotuba yake alijichanganya kido aliposema wachagueni wabunge wa Chadema ili kwenye kikao cha bajeti cha Julai mwakani wapige mapanga bajeti tupate fedha za elimu na mengineyo. Dr Slaa alisahau kuwa yeye ndiye atakayeunda Serikali na lazima aonyeshe kwa wapiga kura kuwa ndivyo itakavyokuwa. [/QUOTE]

Yaap! Kama Rais angependa kuongoza nchi yenye Bunge Active sio mandondocha kama wa CCM.

- Anaongea kwa staili ya kimahubiri. Ana uzoefu katika hilo. Kuna wakati anayaacha matokeo ya anachoongea kwa Mungu na watu. [/QUOTE]

kimahubiri!!?? unaenda wapi?


- Ametokea ndani ya CCM.
Anafahamu kuwa walio wengi anaowahutubia kwa kawaida ni wapiga kura wa CCM. [/QUOTE]

Walio wengi kwa kawaida!!??? angalia takwimu zako vizuri...wapiga kura walio wengi hawana vyama....iwe Iringa au msoga.


- Anatoa maagizo, anatoa siku saba.. hata kabla hajaingia Ikulu. Labda angetamka zaidi " CHADEMA tunataka'. Kuna wapigakura wanaohofia kumwingiza madarakani mwenye silika za udikteta.[/QUOTE]

No no no....kuna wengine tungetamani Sokoine awe Rais ili nchi inyooke.....lakini kwa wanaojificha kwenye uzembe na kulegalega hawapendi watu wa namna ya Sokoine au Dr. Slaa wakamate nchi.

- Dr Slaa hakuzungumzia KATIBA na umuhimu wa kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika KATIBA mpya kwa nchi yetu. Wapiga kura wengi leo wameanza kuelewa kuwa KATIBA yetu ni chanzo cha matatizo yetu mengi. [/QUOTE]

Mmmh!!!! hawahawa wa sera za mifagio na makwanja...wasioelewa EPA na Richmond...leo wanaelewa Katiba??? Hivi wewe mwenyewe mkuu katiba umeisoma mara ngapi na kuielewa??? na rafiki zako wa karibu je? si ajabu wengine hata kuinusa tu hawajawahi japo imejaa kwenye bookshops na hata humu mitandaoni. Please please mkuu Maggid lets be real.

- Huenda Dr Slaa hapati muda mwingi wa kutafuta taarifa zenye kuwagusa watu walio mbele yake kumsikiliza. Na ajabu kubwa kabisa; Dr Slaa tangu mwanzo hadi mwisho wa hotuba yake hakutamka jina la " Mama Monica Mbega". Mgombea Ubunge wa CCM, Iringa Mjini. Hata mgombea wa CHADEMA Mchungaji Msigwa alipopewa dakika tatu na Slaa aongee, naye hakutamka jina la " Monica Mbega" na kwanini wana Iringa Mjini wasimchague Monica Mbega.[/QUOTE]

Why should you mention the name of your looser Girl friend while wedding your wife!!!! sorry nothing personal....lakini unajisikiaje mkeo au mumeo akitaja jina la mtu mwingine wakati wa majambo!!?? Any way suala ni kuwa Monica siyo tishio kwa CHADEMA wala wapinzani....labda angekuwa Mwakalebela hapo angetajwa sana tu maana anatisha.

Tatizo la CHADEMA na vyama vingi vingine vya upinzani linabaki pale pale; oganaizesheni. Wengi katika umati ule uliokusanyika pale Mwembetogwa hawajui zilipo ofisi za CHADEMA mjini.
mjengwa[/QUOTE]

Hilo ni tatizo la CCM. Huwezi kuifananisha CHADEMA na CCM kwenye Organization. Hivi mgombea Urais anapopanda jukwaani na kuuinua mkono wa mtuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya watanzania huku kesi ikiendelea mahakamani dhidi yake na kusema huyu ni mtu safi....hiyo ni Oganaizesheni????? kuna Order hapo?????

Hata hivyo big up sana Maggid you are critical.....as well though as a little 'moved'.
 
Mimi nadhani mjadala ungekuwa mzuri kama Bw. Maggid angepitia ilani ya Chadema na kutuambia mapungufu yake kulinganisha na ile ya CCM. Kwa sababu kusema kuwa Dr. Slaa hakuzungumzia mabadiliko ya Katiba haina maana Chadema haina mpango wa kufanya mabadiliko ya Katiba kwani imeanishwa kwenye Ilani. Kwa CCM mpango kama huo haupo kwa hiyo ni wazi Chadema wanaajenda ambayo wananchi wanaihitaji zaidi (tukiyaamini maneno yake) kuliko alichosema JK pale Iringa.
 
Maggid,

Sikufahamu kuwa wewe ni Mwalimu. Sasa kila kitu kiko wazi.

Ki-mbwa cha Manzese kimeshaeleweka. Lazima nikiri kuwa habari zako hapa JF zinafungua watu macho zaidi. Tumesoma maelezo mengi zaidi kutokana na uchokozi wako. Kama ingelikuwa makala kama ya Ngurumo basi wengi tungeishia kuweka Thanks na kuondoka.

Nafikiri kuna uandishi wa aina mbili. Mmoja ni ule wa KIMAHUBIRI ambao mwisho hamna swali wala nini. Huu ni sawa na anachokifanya Ngurumo. Huo ndiyo ule ambao wengi wamejikita hapa wakidai uende ndani zaidi katika uchambuzi wako. Huo unakuwa umetafuniwa kila kitu na wewe ni kumeza tu.
Mwingine ni huu wako wa kutoa nusu na kuacha nusu nyingine watu wajadili. Huu hata Mwanakijiji huufanya sana hapa. Samahani mie siyo mwaandishi wa habari wala Mwanasiasa na hivyo naweza kuwa nimekosea.

Mwisho lazima nikiri kuwa, baba anayempenda sana mtoto wake, huanza kumfunza kupambana na dunia hii na matatizo yake. Ukiona mtoto kadekezwa kwa kuachiwa afanye kila kitu na kupewa kitu chochote anachokitaka, basi huyo mtoto ataishia kuwa Paris Hilton.

Maggid mtani wangu, endelea kuleta vitu vya Chadema na Slaa peke yake. Hivyo vyama vingine kwa Tanzania inaanza kuwa Historia kidogokidogo.
 

Lakini assumptions zako zinahitaji utafiti: umeafahamu vipi kuwa umati ule hauzijui ofisi za Chadema na makada wake? Je, huo umati uliofurika hapo ulipataje habari za mkutano wa Dr. Slaa? Acha kuongea kama Lt. Gen. Shimbo bwana!
 

kwa kweli mjibu maana maana ni changamoto kubwa katoa ,

ningependa kua unajibu CHANGAMOTO ZA JMushi Otherwise utakuwa mnafiki wa ukweli
 
Right article on a wrong site.truth is strictly prohibited with majority of members inside here.
but thanks, at least they will see it though they wont beleave

 

Mtani wangu Sikonge,

Hakika Wanyamwezi ni watu makini na wenye uelewa mkubwa, ni bahati mbaya tu mtani wangu Lipumba haeleweki na hajui kuwa tatizo ni Uprofesa wake, maana watu anaotaka kuwaongoza wengi ni akina sisi ' ngumbaru'. Kama JF ingekuwa nchi, mtani wangu Lipumba sasa angekuwa anaaga akimaliza awamu yake ya pili huku akimwachia Dr Slaa aendelee kuongoza taifa la JF ( The Land Of Great Thinkers).

Baada ya utani huo hapo juu, nikushukuru sana kwa kunielewa. Ni kweli, ulichokibaini ndio staili yangu hata ninapoandika makala gazetini. Makala zangu kwa kawaida hazizidi maneno mia tisa. Huwa najitahidi kuanza na kisa, kisha naunganisha kisa na ninachotaka kusema. Najaribu sana kutumia lugha nyepesi.

Nataka msomaji anapoiona makala yangu aseme; " Hii makala fupi, ngoje nianze na hii kwanza!" Na anapoanza kusoma anakutana na kisa, ataingiwa na hamu ya kutaka kukimaliza kisa hicho na kuona kina maana gani. Wanasema; facts tell But stories sell!

Basi, msomaji akimaliza kusoma aweze kumsimulia mwenzake alichosoma. Wawili waanze kujadili na wengine wajiunge kwenye kujadili mada. Na mara nyingi hupokea simu za wasomaji wenye kutaka kuniambia mengine zaidi katika nilichokiandika. Kama mwalimu hapo naona nimefanikiwa.
Si mara zote inakuwa hivyo, na isipokuwa hivyo nami hujifunza kutoka kwa wasomaji wangu. Mada niliyowasilisha, huenda imekosa uhalisia. Haiwagusi. Ni hayo tu.
 
Bure kabisa, badala ya kujibu hoja unaleta hadithi hapa?
 
ccm wamebaaanaaa sasa wameachia........nasi tunawachapa nao!
 
Mjengwa ni MPANZI mwerevu.
Ameshagundua habari tunazozitaka hapa ndo ameamua kuelemea huko.
 
MJENGWA Roma haikujengwa na majizi, majambazi, mafisadi. Ilijengwa na uzalendo wa watu wenyewe na watawala. Watawala uanotetea ni wezi, watoa rushwa za uchaguzi na takataka zingine. Dhuruma zao zimefikia mwisho. CCM itatawala daima na milele- mwisho wao ni 31/10/2010. Hujatwaambia vizuri ya kuwa hapo mkutanoni kulikuwa na magari mangapi yaliyokuwa yanawasomba wananchi kuja kuhudhuria mkutano huo. For CCM is a shame! Pole mjengwa ccm ndio hiyo inaondoka madarakani. itachaguliwa mwaka 3000 ukifika. Nina furaha binafsi ya kuwa nategemea kuuona uhuru wa Watanzania baada ya tarehe 31/10/2010 kwa kuwa mwaka 1961 sikuwa duniani.:A S 13:
 
Lakini assumptions zako zinahitaji utafiti: umeafahamu vipi kuwa umati ule hauzijui ofisi za Chadema na makada wake? Je, huo umati uliofurika hapo ulipataje habari za mkutano wa Dr. Slaa? Acha kuongea kama Lt. Gen. Shimbo bwana!

Mwanamayu,

Ninaomba kumuunga Majjid kukili kuwa Chadema na vyama vingine vya upinzani bado hawajalifanyia kazi suala la oganizesheni. Mimi nilijiandikisha kupitia njia ya simu mwaka mmoja sasa na niliahidiwa kuwa viongozi wa eneo ninalokaa watanipigia, mpaka leo sijawahi kupigiwa na wala sijui ofisi za kata ya Kibamba za Chadema zilipo, na hapa tunaongelea Dar es Salaam, kwenye jimbo la naibu katibu mkuu Mnyika.
Je kwenye majimbo ambayo hawajasimamisha hata wagombea iko je????
 
hivi wanakulipa shilingi ngapi kuandaa hizi porojo zako?
 
Kilichonifurahisha mimi hakukuwa na mafuso wala yale mabasi makubwa....watu wamekuja wenyewe....yaani ni watu wa pale Iringa sio wakuletwa kutoka Makete kama CCM wanavyofanya
 
Iko poa..!
Ila uwe pia unatoa analysis ya CCM...
Hasahasa mgombea wake strenght na weakness zake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…