Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Makala hii nilimwandikia Dkt. Bashiru Mei 30, 2018. Nikimkaribisha katika siasa za CCM, nikamuonya, Bahati mbaya maonyo yangu yalipuuzwa, Jibu amelipata...!
_____________
KARIBU KATIKA SIASA CHAFU DKT BASHIRU ALLY, ILINDE AKILI YAKO WAKORA WASIKUPORE, ZINGATIA CCM NI ILEILE.
30 May 2018.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Ninafikiri Ndugu Bashiri Ally kama mtendaji mkuu mpya wa chama cha Mapinduzi, anaufahamu mkubwa juu ya chama cha siasa na dhana ya msingi ya chama, lakini bahati mbaya hana uzoefu wa siasa chafu za CCM, basi iwe hivyo atatumia weledi wake kukitoa chama hicho kwenye mikono ya chama dola na kukifanya chama cha kidemokrasia, akikubali kumezwa atabaki historia kama mzee Mkama.
Ni ukweli usiopingika kwamba ccm inawajibu wa kuruhusu mwelekeo wa siasa za nchi kwasabu ndio imeunda serikali, lakini hilo sio tiketi ya asilimia miamoja ya umiliki wa siasa za nchi, kwakuwa CCM ilizaliwa itakufa, serikali iliundwa na itapita, lakini Tanzania ipo na itadumu daima, yeyote anadhamana ya mwrlekeo wa nch yetu. Dhana yangu ni moja tu kwamba ccm inayo fursa adhimu ya kuanzisha mchakato wa mageuzi nchini na mageuzi yakatokea bila mbinyo wa umma ambao maranyingi huenda sambamba na umwagaji damu.
Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Sura ya Pili, Uk 457 hadi 465 nimeeleza juu ya mageuzi ya mwelekeo wa nchi katika mzizi wa msingi ambao ndio injini ya nchi nao ni muundo wa ujasusi nchini, nanukuu sehemu ya kitabu hicho "Wajibu wa Ujasusi wa ulimwengu wa kileo hasa ujasusi wa kidola ni kuhakikisha mwelekeo wa taifa lolote lile kisiasa, unarandana na malengo mtambuka ya ujasusi huo. Taasisi ama Idara ya Ujasusi ni wajibu wake kuelekeza mwelekeo wa siasa za taifa hilo kwa kutafakuri siasa za mataifa jirani ama ya ulimwengu mpya, mila na desturi za jamii hiyo. Si hayo tu, bali kutafsiri ipasavyo nini maana ya siasa.
Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhakikisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/ madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa, anazitumia kwa maslahi ya nani? Siasa ni mambo mengi lakini sio sayansi. Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka.
Kifilosofia, mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa ama umo katika siasa. Lakini, ili ifanyike siasa lazima pawepo na itikadi. Hivyo, Taasisi na Idara za Ujasusi wa kidola zina jukumu la kutafsiri itikadi pia inayoshirikiwa na watu katika jamii husika.
Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kundi la watu fulani. Kuna aina kuu mbili za itikadi: Itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo-maarifa). Itikadi ya Kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na namna ya kuendesha ama kuongoza nchi.
Kwa upande mwingine, Itikadi za Kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi".
Mabadiliko ya uongozi kwa ccm sio mabadiliko ya kimfumo bali ni mabadiliko ya kiumbo tu ambayo yanaiacha ccm ileile iliyoshindwa kubadilika 1992 katika mabadiliko makuu yaliyoacha chama dola kilekile cha 1964 kilichoundwa baada ya kuwa Jamhuri, na ccm hii ya leo inayoelemewa na mabadiliko ya ulimwengu wa dunia ya tatu na katika kudhihiri hilo ni kuwa ccm imebariki na kuamua kuzuia vijana kujadili, kutoa maoni na hata kufikiri juu ya mabadiliko kwa kutumia mitandao ya kijamii kwa kuikosoa serikali ya ccm, haikuishia hapo, bali imeamua kudhibiti vyombo vya habari vyenye misimamo isiyoegemea upande huku ikianzisha mamluki wa habari ambao wajibu wao ni kuandika propaganda na matusi kwa wapinzani tu huku wakihakikishiwa ulinzi na kinga madhubuti ya kutochukuliwa sheria.
Matokeo yake ni upinzani mkubwa inaokabiliana nao leo kila pembe ya nchi kuanzia ndani ya ccm, ndani ya serikali na nje ya ccm, ni upinzani dhidi ya serikali sio ccm tena. Tatizo la msingi la CCM sio mtu, tatizo lao ni kama tatizo la NCHI yetu tu ambayo sio mtu tuliyemhitaji, bali mfumo na muundo wa nchi ambayo inasimikwa katika maandishi yaitwayo katiba. CCM inahitaji katiba mpya itakayokifanya kiwe chama cha siasa, vivyo hivyo Tanzania inahitaji katiba mpya na sio mtu mpya itakayo tenga na kutambulisha kwakuchora mstari mahali pasiasa za vyama na mahali pa nchi..
Siku CCM ikiamua kubadili katiba yake na kutenganisha urais wa nchi na uenyekiti wa chama, kuacha kunajisi vyombo vya dola hasa kutumia uwanja wa siasa badala ya uwanja wa utawala na udola, ndipo CCM kitakuwa chama rasmi cha sissa, kwa sasa ccm inaongozwa kama chama cha kifamilia kinachoamuliwa na mtu mmoja tu akiwaita wapambe wachache wa ndio mzee waende kwake ikulu badala ya Lumumba au Chamwino.
Karibu sana Daktari Bashiru Ally katika ulimwengu wa sissa chafu na propaganda za Lumumba, mlango ulioungilia ndio utakaoutokea, umeingia ukiwa kijana chunga usizeeke mapema, kubwa zaidi ingia na akili yako, ilinde akili yako, wakora wakikupora akili utakuwa zaidi ya Polepole na Prof Kabudi.
Na Yericko Nyerere